Kwastahili hii kweli tutafika?
Sijiu kama Mwandiko hapa utakuwa mzuri
Naweza kusema huyu ndyo Mtemi Class
Wanafunzi wakiwa darasani makini katika kumsikiliza Mwl huku wakiwa wamekaa chini
Baadhi ya sehemu ya Madawati 1050 yakiwa mbele ya shule za Nyangoto na Matare wilayani Tarime tayari kukabidhiwa kutoka mgodi wa ABG North Mara
Mmoja wa Wanafunzi akifurahia Madawati waliyopewa na Mgodi wa ABG North Mara
Mbali na Msaada wa Madaftari na vifaa vya shule kwa baadhi ya wanafunzi wa sekondary Pia Mgodi huo ulitoa Bajaji kwa watu watatu wasiojiweza
Picha ya Pamoja wanafunzi wa Nyangoto na Matare shule ya Msingi
TARIME
SERIKALI imesema kuwa
kamwe haiwezi kumtegemea mwekezaji kwa kila kitu huku baadhi ya Mambo
yanaweza kufanywa na wanajamiii wenyewe katika sehemu huska.
Kauli hiyo ya
Serikali ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tarime Bw John Henjewele katika hafla ya
kukabidhi Madawati kwa baadhi ya shule zinazozunguka mgodi wa Dhahabu wa
African Barrick Gold (ABG) North Mara, Vifaa vya Shule kwa baadhi ya wanafunzi
na baiskel ya Magurudumu matatu kwa watu watatu wasiojiweza.
Alisema kuwa pamoja
na Misaada inayotolewa na Mgodi huo kwa Jamii lakini pia serikali inashukuru
Mahusiano Mazuri yaliyopo katika Mgodi huo wa African Barrick Gold (ABG ) North
Mara na Jamii.
Mkuu wa Wilaya huyo
aliushukuru Mgodi huo kwa kugundua hali ya Walemavu,kutoa vifaa vya Elimu huku
akisema hiyo ni hatua moja mbele katika kuisaidia Jamii.
“Kwanza
tushukuru sana Mahusiano yaliyopo kati ya Mgodi huu na Jamii lakini pia
hatuwezi kumtegemea Mwekezaji kwa kila Jambo lazima sisi wenyewe tujitoe katika
kufanikisha baadhi ya Mambo yetu” alisema Mkuu huyo wa wilaya.
Akimkaribisha Mkuu
huyo wa Wilaya Meneja mkuu wa Mgodi wa African Barrick Gold (ABG)North Mara Bw
Gary Chapman,alisema Mgodi huo ni miongoni mwa Migodi Afrika ambayo imekuwa
ikiwekeza katika Jamii hasa katika suala la Elimu,Afya,Maji na Maendeleo katika
Jamii.
Alisema Pamoja na
kutotimiza mahitaji kwa shule za Sekondary kwa asilimia mia lakini watajitahidi
kushirikiana na Jamii jiyo katika kujiletea Maendeleo.
“Mgodi huu ni
moja ya Mgodi Afrika ambao unajitolea katika kusaidia Jamii hasa katika
Elimu,afya,maji na Masuala la Maendeleo,lakini pamoja na kutotimiza Mahitaji ya
Jamii kwa asilimia kubwa bado tutaendelea kushirikia na nao” alisema Bw Gary
Chapman
Aidha Uongozi wa
Mgodi huo wa African Barrick Gold umetoa Madawati zaidi ya 1000 kwa shule za
Nyangoto na Matare zilizopo katika eneo la Nyamongo wilayani Tarime Mkoani Mara
huku Miradi yote Mitatu ya Elimu,msaada ya Baiskel na Madawati hayo ikigharimu
kiasi cha shilingi milioni 188.
Watu waliopewa
Baiskel hizo za Miguu mitatu ni pamoja na Eliza Mwikwabe ambaye ni
mfanyabiashara ndogondogo,Penina Mseti muuza mboga na Nyanya pamoja na Gesongo
Chacha ambaye ni fundi wa kuchomelea vyuma.
Taarifa zinasema kuwa
Mgodi huo wa African Barrick Gold (ABG) North Mara umetenga zaidi ya shilingi
Bilion 20 katika kipindi cha miaka mitatu kusaidia Makundi mbalimbali ya
Kijamii yanayozungukwa na Mgodi huo katika kuyaletea Maendeleo
Awali akisema Risala
kwa Mgeni Rasmi Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Nyangoto Bw Ghati Keraryo
alisema kuwa shule zote mbili za Nyangoto na Matare zina jumla ya
Madawati 202 kati ya 654 ambayo yanahitajika.
Alisema kwa niaba ya
Walimu wa shule hizo wanapenda kutoa shukurani kwa Mgodi wa ABG North Mara kwa
kutambua Umuhimu wa Changamoto moja wapo zinazokabili shule hizo ikizingatiwa
kwamba shule hizo zipo karibu na Mgodi huo.
Mbali na Msaada huo
wa Madawati kwa shule hizo,Msoma risala huyo alisema kuwa bado shule hizo
zina upungufu wa Viti 46 na meza 18,huku akiuomba Mgodi huo kuendelea kujenga
Shule hizo kama Mkataba ulivyoainisha katika ya Kijiji na Mgodi.
No comments:
Post a Comment