Majeshi ya Polisi Barani Afrika kushirikiana
kukabili magenge ya kihalifu
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar
ZANZIBAR JUMATANO SEPTEMBA 12, 2012.
Mashirikisho mawili ya Majeshi ya Polisi Barani Afrika yamekubaliana
kuunganisha nguvu za pamoja katika kukabiliana na Magenge makubwa ya
kihalifu wa kimataifa ukiwemo ugaidi, uharamia na biasashara haramu ya
dawa za kulevya.
Mashirikisho
yaliyofikia makubaliano hayo ni SARPCCO ya Majeshi ya Polisi kwa nchi
za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na EARPCCO ya
Majeshi ya Polisi ya nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika (EAC).
Wakitiliana
saini makubaliano hayo mjini Zanzibar, Wakuu wa Mashirikisho hayo, Mkuu
wa Jeshi la Polisi hapa nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema wa SARPCCO
na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Rwanda Kamishna Jenerali Emmanuel
Gasana wa EARPCCO, wamesema hatua hiyo ni mwanga mpya katika kudhibiti
uhalifu unaovuka mipaka kwa nchi za bara la Afrika.
Akizungumza
kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi hapa nchini, Kamishna Msaidizi
Mwandamizi SACP Husein Laiser, amesema kwa muda mrefu sasa genge moja la
kihalifu kutoka nchi zilizopo katika shirikisho moja hushirikiana na
magenge mengine ya upande mmoja jambo ambalo amesema nivigumu kwa nchi
moja kuyakabili kwa urahisi.
Amesema
kwa mfano gari ama madawa ya kulevya yanaweza kusafirishwa kutoka nchi
moja kwenda nyingine na msafirishaji akaungana na kundi lingine katika
nchi ya ugenini pasipo shaka ya kukamatwa kwa urahisi.
Kamanda
Laiser amesema ushirikiano huo utakuwa ni daraja la kusaidia kuwakabili
kwa pamoja watuhumiwa kama hao ambao wengi wao wamekuwa wakiungana na
wenzao katika mataifa mbalimbali kufanikisha uhalifu wao.
Naye
ACP John Bosco Kabera, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini Rwanda, amesema uamuzi huo uliofikiwa utasaidia kwa kiasi
kikubwa katika kukabili matukio ya kihalifu katika ukanda huu wa nchi za
Kusini na zile za maziwa Makuu.
Shirikisho la Majeshi ya Polisi kwa nchi za Maziwa makuu na Pembe ya Afrika SARPCCO, inajumuisha nchi 12
ambazo ni Rwanda, Buurundi, Uganda, Kenya na Tanzania, na zile zilizopo
katika Pembe ya Afrika ambazo ni Sudan, Shelisheli, Ethiopia, Eritrea, ,
Djibouti, Sudan na Somalia.
Na
Shirikisho la Majeshi ya Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika zipo 15
zikiwemo nchi za Tanzania na Shelisheli ambazo zote zinaingia katika
Mashirikisho yote mawili ya nchi za Kusini mwa Afrika na zile za Maziwa
Makuu na Pembe ya Afrika
Nchi
nyingine ni Angola, Afrika ya Kusini, Congo DRC, Lesotho, Msumbiji,
Mauritius, Madagascar, Swaziland, Botswana, Malawi, Zambia, Zimbabwe na
Namibia.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini Rwanda pamoja na ujumbe wake walikaribishwa
kushiriki katika mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kwa nchi za
Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC uliomalizika juzi mjini
Zanzibar.
Mwisho
No comments:
Post a Comment