MUSOMA
WANANCHI Manispaa ya Musoma
mkoani Mara wamelishangaa Jeshi la Polisi mkoani humo kuzuia Maandamano ya
Amani ya Waandihi wa Habari hapo jana .
Wakiongea kwa Nyakati tofauti mjini
Musoma,wananchi hao wamesema kuwa waandishi wa habari walitaka kuandamana ikiwa
ni njia ya kupinga mauaji ya mwandishi mwenzao Daud Mwangosi ambayo
yamesababishwa na Jeshi hilo.
Walisema Askari Polisi wanatakiwa kulinda
amani na si kuzuia maandamano hayo kwani wangekubali kuandamana kwa waandishi
hao nini ambacho kingetokea huku waandishi hao hawazidi hata 50 ina maana hao
Askari hawawezi kulinda watu hao.
“Mimi jana nimeshangaa sana Askari Polisi
kukataza Maandamano ya Amani ya waandishi wa Habari,hawa jamaa walikuwa
wanapinga kuuawa kwa Mwenzao sasa inakuwaje hawa jamaa wanawazuia” alisema Mzee
Jacob Daniel
Alisema kitendo kilichifanywa
na jeshi la polisi mkoani hapa si cha kiungwana hata kidogo kwani maandamano
hayo hayakuwa na uvunjifu wa amani isipokuwa kulani kitendo cha mauaji ya
mwandishi mwenzao kilichotokea mkaoni Iringa.
Mariam Chacha alisema kitendo cha jeshi hilo kuzuia
maandamano hayo ni dhahiri kuwa wanaunga mkono kitendo cha ukatili
kilichofanywa na wenzao mkoani Iringa.
Alisema wananch hatuungi mkono kitendo hicho hata
kidogo”kwakweli tunamshangaa mkuu wa polisi mkoani hapa kutumia madaraka yake
kuwanyima waandishi haki yao ya msingi ya kufanya maandamano ya amani kupinga
mauaji ya mwandishi mswenzao aliyeuwawa kikatili bila hatia’’alisema Chacha.
Juma Mafuru alisema polisi wameshindwa kuzuia
makundi ya uhalifu yanayosumbua wananchi kwa kuwaibia mali zao,kuwakata mapanga
.
Mafuru alisema makundi hayo
yamekuwepo mjini hapa kwa muda mrefu wananchi wamejawa na hofu na makundi hayo.
Hata hivyo aliyataja makundi
hayo yaliyoshindwa kudhibitiwa na jeshi hilo yenye majina ya ajabu kama vile
jamaika moka na mbio za vijiti.
Mapema hapo jana majira ya saa moja asubuhi katika ofisi za Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Mara (MRPC) Waandishi kutoka Wilaya za Mkoa huo walianza kuwasilia kwa ajili ya kutekeleza suala la kuandamana kulaani maauji hayo ya kinyama kwa Mwaandishi huyo wa Habario wa Mkoani Iringa.
Waandishi wakiwa katika mnaandalizi ya kuanza maandamano hayo majira ya saa mmbili na nusu alifika katika ofisi hizo OC CID wa Wilaya ya Musoma Mahamudi Banga kwa niaba ya Mkuu wa Polisi ya Wilaya ya Musoma akiwa na barua yenye kumbukumbu MUS/A.3/VOL 11/.378 ikitaka kuzuia maandamano hayo kwa kwa kile kilichoelezwa katika barua hiyo kuvunja kifungu namba 43(1)ya Polisi na wasaidizi Polisi 2002 ya kutoa taarifa kwa masaa 48.
Katika maandamano hayo Waandishi wa Habari Mkoani Mara wakiwa na mabango walipanga kupita katika barabara za kusaga-Nyerere kupitia NMB na kurudi katika ofisi za chama hicho zilizoo katika jengo la Bodi ya pamba.
No comments:
Post a Comment