Ninayo furaha sana kwa ndugu jamaa, marafiki na wadau wote wa blogs na
vyombo vyote vya habari vya hapa Tanzania, kwani bila nyie ni sawa na
mshumaa kuwaka bila uzi. Hivyo nakubali na kutambua mchango wenu katika
jamii kwani ninyi ndio mnaoifanya dunia kuwa kijiji.
Wadau wote naomba sapoti yenu kwa kuzindua blog yetu ya kijamii inayoitwa JITAMBUE KWANZA yani www.jitambuekwanza.blogspot.com.
Blog hii imeanzishwa na vijana wa kitanzania walioko sehemu mbali mbali
duniani. Jitambue kwanza itazungumzia kwa undani sana
mahusiano katika ndoa, mahusiano kabla na nje ya ndoa, jinsi ya
utunzaji familia, utunzaji wa ngozi, ushauri nasaha, afya na hatari zote
za kijamii zinazopelekea jamii yetu ya kitanzania kudhurika.
Shukurani
zangu za dhati ziwafikie bloggers woote wa Tanzania kwa juhudi zao za
kufikisha habari kwa jamii kwa muda muafaka. Pia pongezi zenu
watangazaji woote mnaohabarisha jamii kwa uharaka zaidi bila kujali ni
usiku au
mchana, pia 100% kwa
Djs woote, kwani bila nyie nchi nzima, kutakuwa hakuna raha. Mwisho
kabisa ni kwa wasomaji woote wa
blogs, kwasababu bila nyie, tunamwandikia nani? hongereni sana na
karibu www.jitambuekwanza.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment