Friday, September 7, 2012

HUKUMU YA AKIYEKUWA MWENYEKITI WA CUF MANISPAA YA MUSOMA YATOLEWA LEO


MUSOMA

MAHAKAMA ya Hakimu mkazi mkoa wa Mara  Leo Imetoa hukumu ya kesi ya jinai  namba 360 ya mwaka 2010  iiliyokuwa ikiwahusu watuhumiwa sita.

Watuhumiwa hao sita wanadaiwa kumteka na kumshambulia vibaya aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha Wananchi CUF wilaya ya Musoma mkoani Mara Bw Didi Musira Koko.

          Bw Didi Musira Koko akiwa hospital baada ya kushambuliwa Mwaka 2010

Katika tukio hilo la kushambuliwa kwa Bw Didi Musira Koko aliyekuwa Mwenyeki wa CUF Manispaa ya Musoma mkoani Mara ilisababisha kuumia  mguu ambapo kwa mujibu wa taarifa za kitabibu ilionekana kuwa mfupa umehama lakini haukuvunjika.

Watuhumiwa katika kesi hiyo  walikuwa ni  Bw Mapinguzi Muhere,Magori  Zembwera na Geofrey Marwa.Wengine ni Justine Dida ,Dickson Anthony na Manumbu Magacha ambapo Mahakama iliwaachia huru watu watano waliokuwa katika kesi hiyo huku Bw Mapinduzi Mhere akikutwa na hatia

Hukumu hiyo iliyosomwa na Hakimu wa Mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa Mara  Hussen Mushi ilitoa adhabu kwa Bw Mapinduzi Mhere kifungo cha Mwaka mmoja Jela au kulipa Faini ya Shilingi laki Tatu

Tukio hilo lililotokea Septemba 25 Mwaka 2010,lilitokea wakati Didi Musira koko akitoka katika mkutano wa kampeni wa aliyekuwa mgombea urais kupitia chama chama Mapinduzi CCM Rais Jakaya Kikwete katika uwanja wa shule ya msingi Mukendo.

No comments:

Post a Comment