WAKUU WA MAJESHI YA POLISI WAKUBALIANA KUDHIBITI UHALIFU WA KIMATAIFA
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar
Wakuu
wa Majeshi ya Polisi kutoka Jumuiya ya Maenedeleo ya Kusini mwa Afrika
SARPCCO chini ya kivuli cha SADC, wamekubaliana kuimarisha nguvu za
pamoja na kukabili uhalifu wa Kimataifa.
Wakuu
hao wa Majeshi ya Polisi kutoka nchi 12 kati ya 14 wanachama wa
Shirikisho hilo, walifikia uwamuzi huo wakati wa mkutano wao wa siku
tatu uliomalizika jana mjini Zanzibar.
Katika
mkutano huo ambao ulitanguliwa na mikutano mingine ya kamati tendaji za
Majeshi hayo walikubaliana pia kubadilishana taarifa za wahalifu na
kuhakikisha kuwa Magenge ya watu wanaojihusisha na uhalifu wa kimataifa
wanabainika na kutiwa nguvuni.
Miongoni
mwa makosa yaliyojadiliwa kwa undani na kupatiwa ufumbuzi wa jinsi ya
kuyakabili ni ugaidi, uharamia, usafirishaji na uuzaji wa dawa za
kulevya pamoja na usafirishaji na biashara haramu wa binadamu.
Wakizungumzia
biashara haramu ya dawa za kulevya, Wakuu hao wamesema biashara hiyo
imekuwa ikileta madhara makubwa kwa vijana walio wengi na hivyo mbali ya
kuthoofisha afya kwa watumiaji, lakini pia dawa hizo zimekuwa
zikithoofisha huduma za kiuchumi kwa nchi masikini.
Wamesema
kutokana na ukweli huo, kuna haja ya kila nchi kuhakikisha kuwa
wanapata taarifa na kuwakamata wale wote wanaojihusisha na usafirishaji,
usambazaji na uuzaji wa dawa hizo.
Wakizungumzia
uharamia, Wakuu hao wamesema kuwa watahakikisha kuwa usalama
unaimarisha katika huba za bahari ya hindi kama hatua ya kudhoofisha
nguvu za wavamizi na watekaji wa meli za bizigo baharini.
Kuhusu
uhalifu unaovuka mipaka, Wakuu hao wa Majeshi ya Polisi kutoka nchi za
SADC wamekubaliana pia kufuatilia nyendo za watuhumiwa wakiwemo wale
wanajihusisha na wizi na usafirishaji wa magari na mifugo ya wizi kutoka
nchi moja kwenda nyingine kwa magendo.
Wakati
wa Mkutano huo, Mkuu wa Jeshi la Polisi hapa nchini Inspekta Jenerali
Saidi Mwema, alichaghuliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Shirikisho la Wakuu
wa Majeshi ya Polisi kutoka nchi zilizo Kusini mwa Bara la Afrika.
Nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Afrika ya Kusini Kamishna Jenerali Bi. Mangwashi Phiyega.
Awali
akifungua mkutano huo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa tanzania
Dk. Mohammed Gharib Bilali, aliwataka Wakuu hao wa Majeshi ya Polisi
kuhakikisha kuwa wanabuni mbinu za kisasa zitakazosaidia kukomesha
uhalifu wa kimaifa ukiwemo ule wa biashara haramu ya dawa za kulevya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi hapa nchini Inspekta Jenerali, Said Mwema, wakati alipowasili kwenye Ukumbi wa mkutano mjini Zanzibar.Baadhi ya washiriki wa mkutano huo kutoka nchi mbalimbali za Shiirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi Kusini mwa Bara la Afrika SARPCCO)Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) akijumuika kuimba wimbo wa Taifa na wakuu wa Jeshi la Polisi Inspekta Generali, Said Mwema (wa pili kushoto) wakati alipofika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar leo Sept 05, 2012 kwa ajili ya kufungua mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wa kujadili uhalifu wa Kimataifa kuhusu madawa ya kulevya na kuimarisha uhusiano kwa nchi za Afrika kiulinzi.Mkuu wa Jeshi la Polisi hapa nchini Inspekta Jenerali, Said Mwema, akizungumza mara baada ya kukabidhiwa uwenyekiti wa Shirikisho la SARPCCO.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wa kujadili uhalifu wa Kimataifa kuhusu madawa ya kulevya na kuimarisha uhusiano kwa nchi za Afrika kiulinzi.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Plisi hapa nchini Inspekta Jenarali, Saidi Mwema. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Afrika ya Kusini, Kamishna Jenerali Bi. Mangwashi Phiyega
--Picha ya pamoja ya Wakuu wa majeshi ya Polisi kutoka nchi za SADC na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
No comments:
Post a Comment