MUSOMA
ZOEZI la Sensa na Makazi mkoani Mara linaendelea Vizuri mpaka sasa licha ya kuwepo
kwa kasoro ndogo tangu kuanza kwake hapo Siku ya Jumamosi usiku chini nzima.
Akiongelea juu ya mwenendo mzima wa zoezi hilo Mratibu
wa Takwimu mkoani Mara Bw. Ramadhani Mbega alisema kuwa mpaka sasa taarifa
alizozipata kutoka sehemu mbalimbali mkoani Mara zinaashiria zoezi hilo kwenda
vizuri.
Alisema Matatizo madogo ambayo yalikuwepo kama
vifaa,picha kwa makarani kama utambulisho yametatuliwa na hivyo zoezi zima
kuendelea kama lilivyopangwa.
“Kulikuwa na matatizo madogo hasa vifaa,picha kwa
makarani lakini kwa sasa hali hiyo imerekebishwa na wanaendelea na zoezi vizuri”
alisema Mratibu huyo
Aidha katika maeneo ya Mbugani na Visiwani,Bw Mbega
alisema kuwa zoezi hilo limeendelea Vizuri kutokana na maandalizi yaliyokuwe
hapo awali na wananchi wa maeneo hayo kuhamasishwa na kupewa elimu ya kutosha
juu ya zoezi la Sense na Makazi.
Mbali na maeneo hao Bw. Mbega alisema kuwa kuna
baadhi ya maeneo ambapo viongozi wa vijiji na vitongoji walikuwa wanalalamika
juu ya maalipo yao na kuongeza kuwa malipo hayo yanatolewa kwa awamu kama
ilivyoagizwa.
Kwa sababu hiyo Mratibu huyo wa Takwimu mkoa wa Mara aliwataka wananchi wote wa Mkoa wa Maraa kuendelea kujitokeza katika zoezi hilo kwani kwa kufanya hivyo wataisaidia Serikali katika kupango mipango ya Maendeleo kwa wananchi.
‘Ya kikubwa mimi naomba wananchi waendelee
kujitokeza katika seku zilizosalia ili tukamilishe zoezi hili vizuri kabisa
kwani kwa kufanya hivyo itakuwa imesaidia miapango ya Maendeleo kwa nchi yetu”
aliongeza Bw Mbega
Mbali na kauli hiyo ya Mratibu wa Takwimu mkoani
Mara Bw Ramadhani Mbega,baadhi ya wananchi ambao wamepata nafasi ya kuongelea
zoezi hilo walisema kuwa mwenendo mzima wa zoeiz la Sense zi mbaya ingawa kuna
baadhi ya Maeneo uelemishaji unaonekana kuwa mdogo
“Mimi naona zoezi linaenda vizuri ingawa kuna baadhi
ya maeneo hali si nzuri sana kutokana na hamasa kuwa ndogo maeneo hayo” Alisema
Juma Omary mkazi wa Kamnyonge mjini Musoma
Hivi karibu akizindua zoezi hilo Mkuu wa mkoa wa
Mara Bw. John Gabriel Tuppa ambaye pia ni Mwenyekiti wa katika ya zoezi hilo
mkoa wa Mara alisema kuwa zoezi hilo halipaswi kuunganishwa na masuala ya dini
kwani lengo la Serikali siyo kujua idadi ya waumini hapa nchini.
Alisema ni vyema watu wakaliunga mkono zoezi hili
kwa asilimia kubwa ili Serikali katika mipango yake iweze kufanikisha kufikisha
Maendeleo kwa Wananchi
No comments:
Post a Comment