Waziri wa Afrika mashariki Samwel Sitta aanza ziara mkoani Kagera lengo kuhamasisha mapokeo kwa wananchi juu ya jumuiya hiyo ya EAC.
Mkoa wa
Kagera unapatikana kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania ambapo Makao makuu ya mkoa yapo katika mji wa Bukoba
umbali wa kilometa 1500 kutoka Dar es Salaam.
Mkoa huu
unapakana na nchi ya Uganda kwa kaskazini, Rwanda na Burundi ,kwa upande wa
magharibi mkoa wa Kigoma, Mwanza kwa upande wa kusini na ziwa Victoria kwa
upande wa mashariki.
Vile vile mkoa wa Kagera uko kusini mwa ikweta
kati ya 1 “00” na 2”45” latitudi. Kwa Iongitudo uko katika nyuzi 30”25” na
32”40” Mashariki mwa ‘greenwich'.
Mkoa wa
Kagera ulijulikana kama “Ziwa Magharibi” jina hili lilidumu katika kipindi cha
ukoloni na baada ya uhuru mpaka mwaka 1979 baada ya vita kati ya Tanzania na
Uganda.
Waziri wa Afrika
mashariki Samwel Sitta ameanza ziara ya kuzungukia sehemu za mipaka mkoani Kagera
na kukagua hali ya maendeleo na mapokeo ya wananchi juu ya jumuiya hiyo ya EAC.
Mkoa ulipata
jina hili kutokana na mto Kagera ambao hutiririsha maji yake kutoka Rwanda
kupitia kaskazini na kumwaga maji yake katika ziwa Victoria.
Mkoa wa
Kagera una jumla ya eneo la kilomita za mraba 39,168 kati ya hizo kilometa za
mraba 28,513 ni eneo la nchi kavu za kilomita 10,655 ni eneo la maji.
Ukiacha
mbali wilaya za Biharamulo na Chato ambazo ni tambarare sehemu kubwa ya mkoa ni
yenye milima na vilima vilivyogawanywa na mabonde yenye matingatinga.
Upande wa magharibi wa mkoa mito mingi inamwaga maji yale katika mto Kagera ambao nao humwaga maji yake katika ziwa Victoria.
Upande wa magharibi wa mkoa mito mingi inamwaga maji yale katika mto Kagera ambao nao humwaga maji yake katika ziwa Victoria.
Mwana wa Makonda
No comments:
Post a Comment