VIJANA 47 WAKIMBIA CHADEMA
Makete
Jumla
ya vijana 47 waliokuwa wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)
katika kata ya Tandala wilayani Makete wamekihama chama hicho na kujiunga na
chama cha mapinduzi (CCM) katika mkutano wa hadhara uliofanyika katani hapo
Wakizungumza
katika mkutano huo vijana hao wamesema wameamua kwa mapenzi yao kukihama chama hicho kutokana na
kutoelewa sera zake na kujiona wakizidi kurudi nyuma kimaendeleo kutokana na
ahadi walizoahidiwa wakati wanajiunga na CHADEMA kutotekelezeka
Mmoja
wa vijana hao aliyejitambulisha kwa jina la Nahom Dovisiana Sanga amesema
alijiunga na Chadema mwaka 2011 lakini ahadi alizoahidiwa ikiwa ni pamoja na kusaidiwa
kiuchumi haijatekelezwa na ndio maana ameamua kutoka kwenye chama hicho
Naye
Imani Nyamike ambaye ni mkazi wa kata hiyo naye amesema kwa upande wake
amejiona kama amepotea kutokana na kukosa
ushirikiano kwa viongozi wa chama hicho hivyo kujiona mpweke tangu alipojiunga
na chama hicho
“Mimi
napenda kuwaasa vijana wenzangu ambao mmmedanganyika na CHADEMA ndugu zangu huu
ni muda wa kurudi CCM, bibi na babu yangu wapo CCM, baba na mama yangu wapo CCM
na mimi nimerudi CCM na nitakufa ndani ya CCM” alisema Nyamike
Akizungumza
mkutanoni hapo Katibu wa CCM wilaya ya Makete Miraji Mtaturu amesema chama
chake kimefurahishwa na hatua iliyochukuliwa na vijana hao ya kujiunga na CCM
na kusema wao kama chama cha mapinduzi wako tayari kuwasaidia vijana hao na
kuwataka kujiunga na kuwa kikundi kimoja ili waweze kupatiwa mikopo ya riba
nafuu ili wakuze mitaji ya bishara zao
Amesema
kumekuwa na tabia ya baadhi ya vijana kujiunga na vyama vyenye sera za uongo
pasipo kujua madhara yanayokuja kuwapata mbele na huku akisistiza wananchi
waliofika kenye mkutano huo kubakia chama cha mapinduzi ambacho kimepewa
dhamana na wananchi kutekeleza sera zake ndani ya wilaya hiyo
“Ndugu
zangu naomba niseme CHADEMA hawana adabu, hivi hakuna ambayo jema lililofanywa
na CCM hata mkapongeza? Ninyi kila siku ni matusi tu majukwaani, hata kitendo
cha wao kuishi kwa uhuru hadi sasa ni jitihada za serikali ya CCM, bado nalo si
jema kwenu?” alisema Mtaturu
Mtaturu
alitoa bendera za CCM kwa vijana hao na kusema kuwa kwa kuwa tukio hilo la kuhamia CCM limetokea ghafla, atajipanga ndani ya
chama chake kufanya sherehe ya kuwakabidhi rasmi kadi za CCM na kuongeza kuwa
zoezi hilo
litafanywa na uongozi wa mkoa ama taifa
Katika
hatua nyingine Mtaturu aliwataka wananchi hao kuendelea kutoa ushirikiano kwa
makarani wa sensa wanaoendelea na zoezi la kuhesabu watu katani humo kwani zoezi
hilo bado
linaendelea kwa siku saba mfululizo pamoja na wananchi hao kujiandaa kutoa
maoni ya katiba mpya pindi tume ya kukusanya maoni itakapofika katani hapo
Naye
diwani wa kata ya Tandala Mh. Egnatio Mtawa amewashukuru wananchi wa kata yake
kwa ushirikiano wanaompa pamoja na kumuomba katibu wa CCm kusaidia
kushughulikia suala la umeme wa gridi ya taifa kufika katani Tandala
Amesema
huo ni mpango wa siku nyingi wa serikali kuhakikisha umeme unawaka Tandala
hivyo anaombwa kusaidia kuimkumbusha serikali ili mpango huo ukamilike
mapema
No comments:
Post a Comment