Wednesday, August 29, 2012

WANANCHI WABOMOLEWA NYUMBA WAANDAMANA OFISI YA DC TARIME


Dinna Maningo, Tarime.


MAMA mmoja akiwa na watoto wake saba  pamoja na wananchi wengine wawili  wakazi wa kijiji cha Turugeti Kata ya Bumera Wilayani Tarime Mkoani Mara wameandamana  hadi  ofisi ya Mkuu Waliya ya Tarime  wakidai kubomolewa nyumba zao jana  na mtu mmoja  aitwae Manyengo Lautent  baada ya kudai kuwa eneo wanaloishi watu hao si lao bali walivamia.



Wakieleza malalamiko yao mbele ya katibu Tawala  wa Wilaya ya Tarime Hernest Kabohola walisema kuwa mnamo agost 28 majira ya saa 6 mchana  Manyengo Laurent mkazi wa mjini Tarime alifika kijijini hapo akiwa ameongozana na kundi la watu zaidi ya 30 na polisi wa Kituo cha Turugeti na kisha wakaanza kubomoa nyumba zao kwa kile walichodai kuwa watu hao wamevamia  na kuishi kwenye eneo la Manyengo Laurent.



“ Jana majira ya saa 6 Manyengo  alikuja na kundi la watu akachukuwa polisi  wa Turugeti wamebomoa nyumba zetu wanasema tuhame eneo hili tumehamia wakati wa oparesheni vijiji  leo hii naambiwa nihame niende wapi na mi ni mzee! Serikali itusaidie sheria itumike ipasavyo”alisema Gitera Marwa.




Mwita Mkori alisema kuwa anashangaa kuona nyumba yake inabomolewa  kwani hajawahi  kushitakiwa mahali popote  kuhusu eneo hilo lakini nyumba yake imebomolewa  bila taratibu za kisheria kufuatwa licha yakuwa eneo hilo alilimiliki tangu wakati wa oparesheni vijiji mwaka 1974.



Rhobi Ryoba alisema kuwa  kitendo cha nyumba yake kubomolewa na kutakiwa kuachia eneo limeathiri familia yake  kwakuwa hawana mahali pa kuishi yeye na familia yake ambapo kwa sasa wanaifadhiwa na  majirani.



“Nitaenda wapi nawatoto 7 na nina ujauzito mme wangu yuko jela alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja na mahakama ya Mwanzo Tarime  kutokana na tatizo hilihili la Manyengo Laurent, Mahakama ikaamuru nyumba yangu ibomolewe  kuwa eneo si letu leo wamekuja wamebomoa japo eneo hilo tumeishi tangu wakati wa oparesheni vijiji wakati huo manyengo akiishi Dar es Salaamu  baadae akahamia mjini Tarime  na sasa kaja kijijini  anadai eneo ni la babu yake kashitaki mme wangu na kisha amebomoa Naomba msaanda wa Serikali utatue tatizo hili”alisema Rhobi



Katibu tawala wa Wilaya ya Tarime Hernest Kabohola aliwataka wananchi hao kurejea  katika uongozi wa Serikali ya kijiji ili tatizo lao lishughulikiwe  kwakuwa wao ndio wanatambua  eneo kwa uhalisia.



Mtendaji wa kijiji cha Turugeti  Matiko Chegere alisema kuwa  wananchi hao ndio wamiliki halali wa eneo kwani wameishi kwa muda mlefu tangu wakati wa oparesheni vijiji na kuwa anasikitika wananchi wengine kubomolewa nyumba kwakuwa hawajawahi kushitakiwa mahali popote na wala ofisi yake na uongozi wa serikali ya kijiji haukupewa taarifa na Manyengo Laurent  kuhusu ubomoaji wa nyumba,nakwamba eneo si la Manyengo Laurent.



Kamanda wa polisi Tarime/Rorya alipohojiwa kama ana taarifa  juu ya polisi wake kuhusika katika zoezi la ubomoaji nyumba alisema ofisi yake haina taarifa hiyo na hivyo kuahidi kufatilia swala hilo kwa ukaribu.

No comments:

Post a Comment