MKUU WA MKOA WA MARA AWAHIMIZA WANANCHI KUJITOKEZA KATIKA ZOEZI LA SENSA
MUSOMA
WAKATI zoezi la
Sensa ya Watu na Makazi likianza nchini kote,tatizo la ukosefu wa Sare maalum
na Vitambulisho kwa Makarani ni miongoni mwa changamoto kubwa ambazo
zimejitokeza katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mara na kusabisha baadhi ya
wananchi kushindwa kutoa taarifa sahihi kwa makarani hao.
Baadhi ya
makarani hao wa Manispaa ya Musoma,Butiama,Rorya na Serengeti kuwa baadhi ya
kaya zimeshindwa kutoa taarifa sahihi kwa madai ya kutowaamini kwa vile tayari
idara ya takwimu ya taifa ilitangaza katika vyombo vya habari kuwa kila karani
atakuwa na sare maalum na kitambulisho cha kazi hiyo.
Mratibu wa Sensa
wa mkoa wa Mara Bw Ramadhan Mbega,amekiri kupata taarifa hizo kutoka maeneo
mbalimbali ya mkoa wa Mara jambo ambalo amesema limetokana na kuchelewa kwa
vifaa hivyo kuwaomba viongozi wa mitaa,vitongoji na vijiji kuwatambulisha
makarani hao kwa wananchi.
Katika hatua
nyingine mkuu wa mkoa wa Mara,Bw John Tupa,amewataka wanancchi
kujitokeza katika zoezi la Sensa na Makazi linaloendelea nchini kote huku
akiwataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Makarani ili kufanikisha
Zoezi hilo.
Mkuu huyo wa
mkoa wa Mara akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhesabiwa katika
makazi yake,amesema zoezi hilo katika mkoa wa Mara limeanza vyema licha ya
kuwepo kwa kasoro ndogo ambazo zinafanyiwa kazi.
No comments:
Post a Comment