Simba B Bingwa ABC Super8 Cup 2012
Kikosi cha timu ya wekundu wa Msimbazi Simba B ambacho kilishuka dimbani hii leo
katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kumenyana na Mtibwa Suger ya
turiani katika fainali za ABC Super8 Cup 2012 na kuwatandika wakata Miwa hao wa miwa wa turiani kwa magoli
4-3.
Simba iliwalazimu kutumia dakika 120 kuwararua wakata Miwa hao walikuwa
wabishi kuwadhibiti Simba hao watoto walio kuwa wakiwatimua kila mara na
mapanga yao ya kukatia miwa.
Kwa matokeo hayo sasa Simba inakuwa timu ya kwanza kunyakua kombe hilo
kwani ndio mara ya kwana kushindaniwa hapa nchini.
Simba iliyochezesha kikosi cha vijana watupu, iliifunga Azam FC iliyojaza
wakali kibao wa kikosi cha kwanza kwa mabao 2-1 ambapo katika mechi iliyotanguliwa na ushindi
mzito wa Mtibwa wa bao 5-1 dhidi ya
Jamhuri ya Pemba.
Mshindi wa
pili wa michuano hiyo ambaye ni Mtibwa amepata zawadi ya Shilingi milioni 20.
Timu mbili
zilizoiishia hatua ya nusu fainali, Azam na Jamhuri, kila moja itapata Sh.
milioni 15 wakati zilizobaki za Super Falcon, Zimamoto na Mtende za Zanzibar
pamoja na Polisi Morogoro ya Bara, zote kila moja itapata Sh. milioni 5
Aidha Mshambuliaji
wa klabu ya Simba B Edward Christopher
ameibuka mfungaji bora wa michuano hiyo ya BancABC Super8 iliyomalizka leo ,ambaye
kabla ya mchezo wa leo alikuwa na mabao matano, katika mchezo wa fainali ya leo
aliweza kufunga hat-trick na kusiadia timu yake kubeba ubingwa huku yeye mwenye
akimaliza akiwa na magoli nane na hivyo kutawazwa kuwa mfungaji bora wa
michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment