Monday, August 20, 2012

         WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA KWENYE SENSA 

TARIME

SERIKALI wilayani Tarime,imewataka wananchi kujitokeza katika zoezi la SENSA ya Watu na makazi  na kwamba haitasita kuchukua hatua kali kwa watu  watakaobainika kushawishi wananchi na kuacha kuhesabiwa katika zoezi hilo linalotarajia kufanyika kuanzia Agosti 26 mwaka huu.

Mkuu wa wilaya ya Tarime Bw John Henjewele,ametoa kauli hiyo wakatiakizunghumza  ofisini kwake ,ambapo amesema kuwa kuna njama ambazo zimeanza kufanywa na baadhi  watu kwaajili ya kupinga Sensa huku wakitumia baadhi ya wazee wa mila.
Kwa sababu hiyo mkuu wa wilaya ya Tarime,amesema kuwa kamwe Serikali haitawavumilia  mtu ama kikundi cha watu kitakabainika kuvuruga zoezi la sensa huku wakijua zoezi hilo limeligharimu taifa fedha nyingi.

Nao baadhi wenyeviti wa vitongoji,mitaa na kata katika wilaya ya Tarime wakizungumza kwa nyakati tofauti wameomba  kupatiwe semina na mafunzo ili waweze kuhusika kikamilifu katika zoezi hilo wakishirikiana na makarani ambao watapangwa katika maeneo yao.

  WANANCHI BUTIAMA WASHINDWA KUUZA PAMBA
MUSOMA

WAKULIMA wa vijiji zaidi ya saba katika kata ya Bisimwa na Buruma katika wilaya mpya ya Butiama wameshindwa kuuza pamba yao hadi sasa baada ya kukosa wanunuzi wa zao hilo.

Wakulima hao ni wa vijiji vya Nyabaikwabi,Bisumwa na Nyamajojo katika kata ya Bisumwa  na  vingine vya kata ya Buruma katika  wilaya hiyo mkoani Mara.
Akizungumza kwa njia ya simu mwenyekiti wa serikali ya kijiji Nyabekwabi Bw Mwita Machogu kwa niabaya wenzake,amesema wananchi wa vijiji hivyo wako katika hatari ya kukumbwa na baa la njaa baada ya kushindwa kuuza zao hilo msimu huu.

Amesema  tangu wananchi wa vijiji hivyo wavune zao hilo la Pamba hawajapata Mnunuzi na hivyo kupelekea hali yao ya Maisha kuendelea kuwa ngumu siku hadi siku huku wananchi hao wakiwa wametumia fedha nyingi kulima zao hilo.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo serikali ya kijiji cha Nyabaikwabe,amesema kuwa mbali na zao la Pamba lakini pia zao la Mhogo kwasasa limekumbwa na ugonjwa ambapo unasababisha zao hilo kuoza likiwa ardhini.

Amesema hatua hiyo inasababisha debe moja la Zao hilo Muhogo kuuzwa kuazia shilingi elfu saba mpaka elfu nane hivi sasa,huku diwani wa kata ya Bisumwa Bw Magina Magesa akikiri kuwapo kwa hali hiyo ambayo imewaathiri wakulima.

    VYOMBO VYA HABARI VYAOMBWA KUTANGAZA HABARI ZINAZO CHOCHEA MAENDELEO
TARIME
UONGOZI wa halmashauri ya wilaya ya Tarime,ameviomba vyombo vya habari kuandika na kutangaza habari  katika wilaya hiyo ambazo zitachochea kasi ya mandeleo pamoja na kuibua changamoto zinaibili jamii badala ya kuchochea na kutisha wawekezaji kwa kuandia habari mbaya pekee.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo ya Tarime Bw Amos Sagara,ameyasema hayo mjini Tarime wakati akizungumza na waandishi wa habari,ambapo amesema vyombo vya habari vina nafasi kubwa ya kuchochea maendeleo kwa kuibua kero zinazowakabili wananchi hasa wa maeneo ya vijijini na kupatiwa ufumbuzi.

Hata hivyo ameonya kamwe waandishi wa habari waepuke kuandika habari kwa maslahi ya mtu ama itikadi ya vyama vya siasa jambo ambalo amesema ni kinyume cha fani hiyo hatua ambayo pia inaweza kusababisha uhasama katika jamii.

Amesema tayari halmashauri hiyo imeagiza watendaji wake kutoa taarifa kwa waandishi wa habari kila wakati kwa kuelezea mafanikio,changamoto pamoja na kero mbalimbali wanazo kumbana nazo katika utendaji wa wa kazi na zile zinahusu wananchi katika maeneo yao.
Kwa upande wao waaandishi hao wa habari hasa wa wilaya ya Tarime wamemueleza kiongozi huyo jinsi wanavyobaguliwa na kutoshirikishwa  katika baadhi ya vikao vya halmashauri hususani ziara mbalimbali za viongozi ndani na nje ya mkoa wa Mara jambo linalowanyima fursa ya kuandika habari za maendeleo katika wilaya hiyo.

No comments:

Post a Comment