BUTIAMA
WATANZANIA
wametakiwa kuchukia vitendo vya rushwa,ubaguzi,ukabila,udini na ubinafsi
ili kulinda amani ya nchi ikiwa ni njia moja wapo ya kumuenzi kwa vitendo baba
wa taifa Hayati Mwalimu Julius Kabarage Nyerere.
Hayo yamesemwa
kijijini Butiama mkoani Mara na kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa
mwaka huu Bw Honest Ernest Mwanonossa,mbele ya kaburi la baba wa taifa, baada
ya kuwasha Mwenge wa Mwitongo nyumbani kwa baba wa taifa hayati mwalimu Julius
Kambarage Nyerere katika eneo la Mwitongo.
Amesema kuna
baadhi ya viongozi nchini wameshindwa kumuenzi Baba wa taifa kwa kukemea kwa
vitendo matumizi ya ukabila,udini na rushwa hasa katika siasa jambo
ambalo ni hatari na kwamba vitendo hivyo visipothibitiwa mapema vinaweza
kuhatarisha amani ya nchi.
Akiwa kijijini
Butiama, kiongozi huyo wa mbio za mwenge kitaifa,ameweka jiwe la msingi
katika jengo la wodi ya wazazi na watoto ambalo linajengwa kwa ushirikiano wa
wananchi wa kijiji cha Butiama,Halmashauri ya Musoma vijijini na Serikali
kuu kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 483 kama sehemu ya kuongeza miundo
mbinu katika hospitali hiyo inayotarajiwa kuwa ya wilaya mpya ya butiama.
Awali viongozi
hao wakiongozwa na kiongozi huyo wa mbio za mwenge kitafa,wamepata fursa
ya kuomba na kuweka mashada ya maua katika kaburi la baba wa taifa hayati
mwalimu Julius Nyerere.
No comments:
Post a Comment