UAMSHO
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi- Zanzibar
ZAIDI ya wafuasi 40 wa kikundi cha Jumuiya ya
Uamsho Zanzibr wamekamatwa na Polisi kufuatia vurugu zilizotokea jana
kwenye eneo la Darajani mjini Zanzibar.
Kamanda wa
Polisi mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar ACP Aziz Juma Mohammed, amesema
kuwa watuhumiwa hao walikamatwa baada ya kufunga barabara kadhaa kwa
mawe, vyuma, matofari na kuchoma moto matairi ya magari.
Kamanda
Aziz amesema kuwa katika vuurugu hizo hakuna Askari ama watuasi wa
kikundi hicho waliofariki ama kujeruhiwa wakati wa ghasia hizo
zilizokuwa nimeendelea katika mitaa mbalimbali ya mji wa Zanzibar.
Amesema
wafuasi hao walitumia mawe, chupa na vipande vya mbao kuwarushia Polisi
lakini amesema hadi kumalizika kwa zoezi la kuwatawanya wafuasi hao saa
nane usiku wa kuamkia leo, (jana).
Hata hivyo
Kamanda Aziz amesema bado Jeshi la Polisi linaendelea kuwasaka viongozi
wa kikundi hicho ambao wametoroka mara baada ya kuibuka kwa vurugu hizo.
Amesema
vurugu hizo ambazo zilianza jana majira ya saa 11.00 jioni, zilidumu
hadi saa 8.00 usiku kufuatia wafuasi wa kikundi hicho kujikusanya katika
maeneo mbalimbali wakifanya vurugu.
“Tunawatafuta
viongozi wa kikundi hicho na tunawataka popote walipo wajitokeze na
kujisalimisha wenyewe Polisi.” Alisema Kamanda Aziz.
Mara baada
ya kuanza kwa ghasia hizo na hadi asubuhi ya leo (jana) barabara za
Darajani na mlandege, mitaa iliyokuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu,
ilikuwa haia hata mtu mmoja na hata biashara zilisimama.
Hata hivyo
biashara mbalimbali zimerudia tena katika hali yake ya kawaida huku
watumishi wa Baraza la Manispaa ya mji wakiendelea na kazi ya uongoaji
wa mawe, matofari na mabaki ya majivu ya matairi ya magari.
Ametoa wito
kwa wananchi kutoa taarifa Polisi endapo watawaona ama kubaini mahala
walipojificha viongozi wa kundi hilo la uamsho ili wahojiwe kwa tuhuma
za kuanzisha ghasia.
No comments:
Post a Comment