GREDA LAGONGA MWENDESHA PIKIPIKI MJINI MUSOMA JIONI YA LEO NA KUSABABISHA KIFO
Ajali
mbaya iliyohusisha Greda na Bodaboda imetokea leo mjini Musoma
katika makutano ya Barabara ya Shabani na Bus Stop.
Ajali hiyo
imepelekea abiria aliyekuwa amepakiwa katika pikipiki hiyo kujeruhiwa
vibaya maeneo ya tumbo baada ya kuburutwa na mashine hiyo ya
kutengenezea barabara.
Hata hivyo limetokea gari la shirika la umeme
Tanesco na kumchukua majeruhi huyo na kumkimbiza katika hospitali ya
Mkoa wa Mara.
Mpaka mwandishi wetu anaondoka eneo la tkio kulikuwa na
sintofahamu ya ni wapi dereva wa pikipiki na greda hilo walipoelekea
kwani mashuhuda wa tukio hilo wanasema dereva wa pikipiki alikimbia
punde tu ajali ilipotokea.
Taarifa ambazo Mwana wa Afrika amezipata na kuthibitishwa na baadhi ya Marafiki ni kwamba dada huyo amefariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa hospital
No comments:
Post a Comment