Tuesday, February 14, 2012

KATIKA KUSHEREKEA KOMBE LA AFRIKA WAWILI WAFA LUSAKA

Watu wawili wamekufa na wengine 35 kujeruhiwa mjini Lusaka, Zambia kufuatia sherehe za ushindi wa timu ya mpira wa miguu ya nchi hiyo kutwaa kombe la mataifa ya Afrika AFCON.


Baada ya dakika 120 za mechi ya fainali kati ya Zambia na Ivory Coast kumalizika bila goli, timu hizo ziliingia hatua ya penati, ambapo mlinzi wa timu ya Zambia Stoppila Sunzu alifunga goli la ushindi lililosababisha sherehe za ghafla katika miji mbalimbali nchini humo. 

Polisi nchini Zambia wanasema ajali 510 zimeripotiwa tangu kuanza kwa mashindano hayo Januari 21

No comments:

Post a Comment