Tuesday, February 14, 2012

HABARI KUTOKA MARA


BUNDA
WAKAZI WA KITONGOJI CHA MBUGANI KILICHOKO KATIKA MAMLAKA YA MJI MDOGO WA BUNDA MKOANI MARA WAMEITAKA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA KUSITISHA MARA MOJA MAOMBI YA KANISA LA ANNE BAPTIST LA MJINI HUMO YA KUTAKA LIMILIKISHWE EKARI 93 ZA ARDHI NA KUTISHIA KWENDA KUMWONA WAZIRI MWENYE DHAMANA KAMA HAITOFANYA HIVYO.
UAMUZI HUO WA WAKAZI HAO UMEFIKIWA KATIKA MKUTANO WA HADHARA ULIOFANYIKIA KATIKA KITONGOJI HICHO NA KUHUDHURIWA NA OFISA ARDHI WA HALMASHAURI HIYO DENIS MASAMI ULITOKANA NA KILE WALICHOSEMA KUTOSHIRIKISHWA KWAO KATIKA MCHAKATO MZIMA WA MATUMIZI YA ARDHI HIYO
KATIKA TAMKO LAO LILILOSOMWA NA FORTUNATUS MARO WAKAZI HAO WAMESEMA KITENDO CHA IDARA YA ARDHI YA WILAYA HIYO CHA KUTOWASHIRIKISHA WAKAZI WA ENEO HUSIKA AMBAO KISHERIA NDIO WAMILIKI WA ARDHI YA ENEO HILO KATIKA KUGAWA SEHEMU HIYO YA ARDHI NI UKIUKWAJI WA SHERIA UNAOPASWA KUEPUKWA NA MAMLAKA HUSIKA ILI KUEPUSHA MIGOGORO YA ARDHI NDANI YA JAMII.

MARO ALIYEKUWA AKISOMA TAMKO ALIENDA MBALI ZAIDI PALE ALIPOSEMA HUENDA MAOFISA WA IDARA YA ARDHI WILAYANI HUMO WAMEPEWA RUSHWA KUTOKA KWA WATU WA KANISA LA ANNE BAPTIST ILI WAWAMILIKISHE KINYEMELA ENEO HILO BILA KUWASHIRIKISHA WANANCHI NA KUSEMA KAMWE HAWAKO TAYARI KUYAVUMILIA MAMBO KAMA HAYO.
KAULI YA HIYO YA MARO ILIUNGWA MKONO NA MWENYEKITI WA KITONGOJI HICHO ARISTARIKO BULAYA ALIYEONESHA MSHANGAO WAKE JUU YA MAAMUZI YA IDARA HIYO YA ARDHI YA KUYAKUBALI MAOMBI HAYO YA KANISA HILO HUKU ARDHI HIYO INAYOMILIKIWA NA WAKULIMA IKIWA BADO HAIJAPIMWA BILA HATA KUWASHIRIKISHA WANANCHI NA KUITAKA IDARA HIYO ISITISHE MAOMBI HAYO MPAKA IAFIKIANE NA WAKAZI HAO.
KWA UPANDE WAKE OFISA ARDHI WA WILAYA HIYO DENIS MASAMI AKIJIBU TUHUMA HIZO AMESEMA WANANCHI WA KITONGOJI HICHO HAWAKUWEZA KUSHIRIKISHWA KATIKA UPIMAJI HUO KWA SABABU ENEO HILO LILILOMO NDANI YA ENEO LA MAMLAKA YA MJI MDOGO WA BUNDA KISHERIA NI MALI HALALI YA MAMLAKA HIYO ..
MAPEMA AKIONGEA KATIKA MKUTANO HUO MWAKILISHI WA KANISA HILO LENYE MAKAO YAKE MAKUU NCHINI MAREKANI MANG'ALARYA MASUBUGU AMESEMA KANISA LAKE LILIFUATA TARATIBU ZOTE ZA ARDHI LIKIWEMO KUTUMA MAOMBI KWA MAANDISHI NA KWAMBA KANISA HILO LITALIPA GHARAMA ZOTE ZA FIDIA ZA WENYE MASHAMBA IKIWA WATAKUBALIWA.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

MUSOMA


WAKAZI WA MANISPAA YA MUSOMA MKOANI MARA WAMETAKIWA KUZINGATIA KANUNI, SHERIA NA TARATIBU ZINAZOWEKWA NA MANISPAA ILI  KUUFANYA MJI HUO KUWA SAFI NA MANDHARI INAYOVUTIA

WITO HUO UMETOLEWA NA MKURUGENZI WA MANISPAA YA MUSOMA NATHAN MSHANA WAKATI AKIONGEA NA KITUO HIKI  LEO ASUBUHI OFISINI KWAKE KATIKA MANISPAA YA MUSOMA MKOANI MARA

AMESEMA MANISPAA IMEANZA KUFANYA MCHAKATO WA KUWEKA MJI WA  MUSOMA KATIKA HALI YA USAFI KWA KUWEKA MAPIPA YA TAKA SEHEMU MBALIMBALI YA MJI ILI KUZUIA WATU KUTUPA TAKA HOVYO

AMEWATAKA WAFANYA BIASHARA WOTE MKOANI MARA KUWA NA MAPIPA YA TAKA KATIKA MAENEO YA BIASHARA LENGO LIKIWA NI KUZUIA TAKA KUZAGAA KATIKA MAENEO YA BIASHARA ZAO

MKURUGENZI HUYO AMESEMA KUWA KWA SASA BARAZA LA MADIWANI NA WAKUUU WA IDARA SABA WAPO KWENYE SEMINA KATIKA MANISPAA YA MOSHI KWA MADHUMUNI YA KUJIFUNZA  NA KUIMARISHA SHERIA NDOGONDOGO ZINAZOWEKWA NA MANISPAA ILI KUDHIBITI TATIZO LA UCHAFU KATIKA MANISPAA YA MUSOMA

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

BUNDA

MKUU WA WILAYA YA BUNDA FRANSIC ISAAC AMESEMA KUWA HATUA YA SERIKALI WILAYANI HUMO KUWAZUIA WAKAZI WA KATA YA BUNDA STOO MJINI HUMO KUJENGA SEKONDARI YAO ILITOKANA NA SABABU KADHAA IKIWAMO YA KUTOKUELEWANA KWAO SEHEMU YA  KUIJENGEA SHULE HIYO.
AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KWA NIABA YA MKUU HUYO WA WILAYA AFISA TARAFA WA TARAFA YA SERENGETI  JUSTINE LUKAKA AMESEMA KUWA MARA BAADA YA WAKAZI HAO KUAZIMIA KUJENGA SHULE YAO YA SEKONDARI MGOGORO WA SEHEMU YA KUIJENGEA SHULE HIYO ULIZUKA MIONGONI MWAO.
KWA MUJIBU WA OFISA TARAFA HUYO MVUTANO HUO WA SEHEMU YA KUIJENGA SHULE HIYO UNATOKANA NA MUONEKANO  MBAYA WA JOGRAFIA YA KATA HIYO UNAOIGAWA KATIKA SEHEMU MBALIMBALI ZINAZOONESHA KANA KWAMBA SIYO KATA MOJA NA HALI ILIYOPELEKEA WAKAZI WA KILA SEHEMU KUTAKA IJENGWE KATIKA ENEO LAO NA HIVYO KUZUSHA MGOGORO MIONGONI MWA.
MBALI NA HILO PIA AFISA TARAFA HUYO AMESEMA MKUU WA WILAYA ALIFIKIA HATUA YA KUWAKATALIA KUJENGA SHULE YAO YA SEKONDARI KWA KUWA HOJA HIYO ILIKUJA HUKU BARAZA LA MADIWANI LA HALMASHAURI YA WILAYA HIYO LIKIWA LIMESHAPITISHA AZIMIO LA KUONGEZA VYUMBA VYA MADARASA 88VINAVYOHITAJIKA  KATIKA SHULE 24 ZA SEKONDARI ILI KUWAWEZESHA WATOTO WOTE 5325 WALIOFAULU NA KUOSWA NAFASI WAENDE SEKONDARI MAPEMA MWEZI UJAO.
LUKAKA AMESEMA MKUU WA WILAYA ANAWASISITIZIA WAKAZI WA KATA HIYO KUENDELEA KUCHANGIA BILA SHURUTI UJENZI WA SHULE ZA SEKONDARI ZA RUBANA NA DR.NCHIMBI WALIZOZIJENGA KABLA YA KUTENGWA KUWA KATA MWAKA 2009 NA AMBAPO WATOTO WAO WANAENDELEA KUSOMEA .
HIVI KARIBUNI WAKAZI HAO WALIRIPOTIWA KUGOMA KUCHANGIA UJENZI WA SHULE HIZO KAMA SHINIKIZO LA KUITAKA SERIKALI WILAYANI HUMO IWARUHUSU WAJENGE YA KWAO HALI ILIYOPELEKEA MKUU WA WILAYA HIYO KUAMURU KUKAMATWA NA KUWAFIKISHA MAHAKAMNI  WENYEVITI  WAWILI WA VITONGOJI WAKITUHUMIWA KUCHOCHEA MGOMO HUO.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

No comments:

Post a Comment