Thursday, December 29, 2011

MAFUTA TABU SANA MUSOMA


MUSOMA

MANISPAA YA MUSOMA MKOANI MARA HAINA KABISA NISHATI YA MAFUTA AINA YA PETROLI HUKU KUKIWA NA UPUNGUFU MKUBWA MAFUTA YA DIZELI HALI AMBAYO IMESABABISHA NISHATI HIYO KUPATANDA KARIBU MARA MBILI YA BEI YA KAWAIDA.

KUTOKANA NA UKOSEFU HUO WA MAFUTA YA PETROLI KUMESABABISHA MAFUTA HAYO KUUZWA KATIKA VICHOCHORO AMBAPO LITA MOJA IMEPANDA KUTOKA SHILINGI 2,060  HADI SHILINGI 3,500 NA 4,000 KWA LITA MOJA.
BAADHI YA WAMILIKIWA WA VITUO VYA  MAFUTA WAMEDAI KUWA HALI HIYO IMEJITOKEZA KUTOKANA NA KUSHINDWA KUSAFIRISHA MAFUTA HAYO KUTOKA JIJINI DAR ES SAALAM HUKU BAADHI YA WANUNUZI WAKIDAI WAMILIKI HAO WA VITUO VYA MAFUTA WAMEFICHA NISHATI HIYO NA KUUZA KWA MTU WANAJUANA KWA KUJIFICHA KWA BEI HIYO KUBWA.
HALI KAMA HIYO PIA IMERIPOTIWA KUZIKUMBA WILAYA ZA BUNDA,TARIME NA RORYA JAMBO AMBALO LIMESABABISHA NAULI KUPANDA MARA MBILI YA BEI YA KAWAIDA.
MKURUGENZI WA MAMLAKA YA UDHIBITI WA MAJI NA NISHATI EWURA BW HARUNA MASEBU AKIONGEA NA VICTORIA FM KWA NJIA YA SIMU AMEKIRI UKOSEFU WA NISHATI HIYO KATIKA MKOA WA MARA AMBAPO AMESEMA TAYARI AMEONGEA NA UONGOZI WA MKOA WA MARA KWA KUWAOMBA MAAFISA BIASHARA WA WILAYA,MKOA NA POLISI KUFANYA UKAGUZI KATIKA VITUO VYOTE KABLA YA KUCHUKULIWA HATUA KALI.
AMESEMA ENDAPO WATABAINI WAMILIKI HAO WA VITUO WAMEFICHA MAFUTA HAYO MAKUSUDI EWURA ITACHUKUA HATUA YA KUWAFUNGIA PAMOJA NA KUWANYANG’ANYA LESENI ZAO MARA MOJA.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

JESHI LA POLISI MKOANI MARA LIMEONYA KUWA KUANZIA SASA HALITAMVUMILIA DEREVA YOYOTE ANAYEENDESHA CHOMBO CHA MOTO KWA KUTUMIA UZOEFU BILA KUPATA  MAFUNZO YANAYOKUBALIKA KUTOKA KATIKA CHUO KINACHOTAMBULIKA NCHINI.
KAULI HIYO IMETANGAZWA NA MKUU WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI RCO MKOA WA MARA SSP EMANUEL LUKULA,WAKATI AKIFUNGA MAFUNZO YA UDEREVA KATIKA CHUO CHA MAMLAKA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI VETA MKOANI MARA.
AMESEMA HIVI SASA KUMEIBUKA KUNDI KUBWA LA MADERAVA WANAOENDESHA MAGARI NA VYOMBO VINGINE VYA MOTO KWA KUTUMIA UZOEFU,JAMBO AMBALO LIMEKUWA LIKISABABISHA AJALI ZA MARA KWA MARA AMBAZO ZIMEKUWA ZIKIGHARIMU MAISHA YA WATU NA KULILETEA HASARA KUBWA TAIFA.
KWA UPANDE WAKE, MKUU WA IDARA YA MFUNZO WA VETA MKOA WA MARA BW LUICE DAVID,AMESEMA NI MATUMAINI YA CHUO HICHO KINACHOMILIKIWA NA SERIKALI KUWA MADEREVA HAO WATATUMIA MAFUNZO HAYO ILI KUPUNGUZA  AJALI ZA BARABARANI AMBAZO MARA NYINGI ZIMEKUWA ZIKICHANGIWA NA MAKOSA YA KIBINADAMU.
KWA UPANDE WAKE MMOJA YA WAHITIMU WA MAFUNZO HAYO BW BONIFASCE MASONGA,AMESEMA SERIKALI INAPASWA KUSIMAMIA SHERIA KATIKA KUHAKIKISHA KILA DEREVA ANAFANYA KAZI HIYO BAADA YA KUPATA MAFUNZO KAMA HAYO TU.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

No comments:

Post a Comment