Tuesday, October 11, 2011

JAMII IMETAKIWA KUTOKOMEZA VITENDO VYA KIKATILI


MUSOMA
JAMII imetakiwa kupambana ili kutokomeza vitendo vya kikatili katika jamii hasa kwa wakati huu ambapo serikali na taasisi zisizo za kiserikali zimeonyesha juhudi katika kupambana na vitendo hivyo.
Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Mara Robert Boaz katika taarifa yake iliyosomwa na na Babu Sanare aliyemwakilisha kama huyo katika ufunguzi wa mafunzo ya ukatili wa kijinsia kwa jamii katika ukumbi wa Anglikana mjini Musoma
Katika taarifa hiyo Kamanda Boaz alisema kuwa ukatili wa kijinsia ni tatizo kubwa katika jamii hivyo kupunguza utekelezaji wa majukumu ya kila siku katika jamii,aidha kamanda alilipongeza shirika la msaada wa kisheria kwa wajane na watoto Centre For Widows and Children Assistance kwa kuwa mshirika mkubwa katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia na kuona umuhimu wa kuandaa mafunzo hayo ya siku tatu.
 “Napenda kulipongeza shirika hili kwa kuwa mdau mkubwa katika katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia na kuona umuhimu wa kuandaa mafunzo haya” ilisema sehemu ya taarifa hiyo
Kamanda Boaz alisema kuwa Serikali inaendelea kufanya jitihada kubwa katika mapambano dhidi ya vitendo vya kikatili wa kijinsia huku akisema kuwa kwa shirika hilo linalofadhiliwa na  Frola Family Foundation kutoka nchini Marekani kuwa msaada mkubwa katika kutokomeza vitendo.
Aidha kamanda alisema kuwa mapambano dhidi ya vitendo hivyo jeshi la Polisi litaendelea kupambana navyo kama shirika hilo lilivyoonyesha jitihada za kupambana na vitendo hivyo ambavyo ni kero katika jamii hasa vikiwa vimekithiri kwa wanawake na watoto.
Akitoa mafunzo kwa washiriki kutoka  taasisi mbalimbali mwezeshaji  AMBAYE NI MWANASHERIA Magdalena Mlolere kutoka kituo cha msaada wa kisheria kwa wanawake (WLAC) alisema kuwa vitendo vya kikatili vimegawanyika katika makundi mbalimbali kama ukatili wa kimwili,ukatili wa kingono, ukatili wa kiuchumi na ukatili wa kiakili.
Alisema kuwa hizo ni aina za ukatili ambapo jamii pengine hazielewi nah ii ni kutoka na ufinyu wa elimu katika jamii lakini wengine wakiwa wanafahamu lakini wanasukumwa na mfumo dume,mwanasheria Mlolore aliongeza kuwa ni vyema jamii ikaelemishwa ipasavyo kuhusiana na vitendo hivyo vya kikatili ili punguza vitendo vya kinyanyasaji katika jamii.
Katika mafunzo hayo ambayo yatamalizika oktoba 13 mwaka huu katika ukumbi huo yameibua changamoto mbalimbali hasa pale washiriki walipokuwa wakihitaji ufafanuzi wa kina kuhusiana na vitendo vya kikatili

No comments:

Post a Comment