Thursday, August 4, 2011

KOCHA JEAN PAULSEN AKITANGAZA KIKOSI CHA TAIFA STARS LEO

 
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 20 kwa ajili ya mechi ya kirafiki ugenini inayochezwa kwenye tarehe zinazotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)- FIFA dates. Mechi itachezwa Agosti 10 mwaka huu.
 
Wachezaji walioitwa kwenye kikosi hicho ni makipa; Shabani Dihile (JKT Ruvu) na Shabani Kado (Yanga). Mabeki ni nahodha Shadrack Nsajigwa (Yanga), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Amir Maftah (Simba), Chacha Marwa (Yanga) na Juma Nyoso (Simba).
Viungo ni Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Juma Seif ‘Kijiko’ (Yanga), Jabir Aziz (Azam), Nurdin Bakari (Yanga), Soud Mohamed (Toto Africans) na Godfrey Taita (Yanga). 
 
Washambuliaji ni Salum Machaku (Simba), Julius Mrope (Yanga), Mrisho Ngassa (Azam), Hussein Javu (Mtibwa Sugar), John Bocco (Azam) na Thomas Ulimwengu (U23).
Timu itaingia kambini kesho (Agosti 5 mwaka huu) jijini Dar es Salaam na itaanza mazoezi siku hiyo hiyo saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume. 
 
Msafara wa timu hiyo wa jumla ya watu 30 utaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano.
 
Timu ya Tanzania (Taifa Stars) imepangwa kundi C Kanda ya Afrika ambalo lina timu za Cote d’Ivoire, Morocco na Gambia. Lakini kabla ya kuingia katika kundi hilo Stars italazimika kucheza raundi ya kwanza ya mchujo dhidi ya Chad. 
 
Stars ikifanikiwa kuitoa Chad baada ya mechi mbili za nyumbani na ugenini zitakazochezwa kati ya Novemba 11-15 mwaka huu ndiyo itaingia katika kundi hilo la C. Pia mshindi wa kundi C ndiye atakayeingia katika raundi inayofuata kabla ya kupata tiketi ya kwenda Brazil

SOURCE Fullshangwe 

No comments:

Post a Comment