Thursday, August 4, 2011

CHUO CHA MIPANGO DODOMA CHAONGEZA TAWI MWANZA

Na Tiganya Vincent, Dodoma _MAELEZO_Dodoma
 
Chuo cha Mipango cha Mjini Dodoma kinatarajia kufungua tawi jipya katika Mkoa wa Mwanza mapema mwezi ujao ili kuongeza udahili wa wanachuo waochukua Astashahaya ya Mipango vijijini.

Hatua hiyo inalenga kuzalisha wataalamu wengi watakaosaidia kuzalisha wataalamu wengi wa sekta ya mipango wataowezesha wananchi kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo kuanzia ngazi ya kijjiji hadi Taifa.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Afisa Masoko na Mahusiano wa Chuo cha Mipango cha Dodoma Godrick Ngoli wakati anaongea na waandishi wa habari mjini Dodoma kwenye Banda la Wizara ya Fedha wakati wa maonyesho ya wakulima ya nane kitaifa yanayofanyika mkoani hapa.
Alisema kuwa kimsingi masomo katika tawi la Mwanza yangeanza Mwezi wa Saba lakini kutokana na utaratibu wa uboreshaji wa miundombinu kwa ajili ya kujifunzia na kufundishia wamelazimika kusogeza mbele hadi septemba mwaka huu ambapo ndio mwaka wa masoko kwa tawi hilo utakapoanza.


Ngoli alisema kuwa katika kuanzia wanatarajia kuchukua wanafaunzi 300 ambao watajiunga na kozi hikwa wale watakaofanikiwa kufaulu vizuri katika mitihani yao ya kila ngazi.


Aidha Afisa huyo alisema lengo la Chuo hicho ni kuanzisha astashahada mbalimbali zinazowiana na shaho la kuzalissha wataalamu waliobebea katika fani za mazingira na mipango ambayo ndio chachu ya kuwasaidia wakulima vijijini kupata mazao mengi.


Ngoli aliongeza kuwa bila kuwa na wataalamu waliobobea katika mipango mizuri ya utunzaji wa mazingira hatuwezi kuwa na kilimo kilichoendelevu.

Alisema kuwa Chuo hicho kimefanyia maboresho mitala yake ili kuhakikisha kuwa nchini kunakuwepo na wanasimia miradi ili kuifanya iwe endelevu badala ya kuwa ya muda mfupi.

Ngoli alisema kuwa mipango mizuri inayotokana na wataalamu walioelimika watasaidia kuharikisha mapinduzi ya kijani nchini.

No comments:

Post a Comment