Thursday, August 4, 2011

IDADI YA WATU NCHINI RWANDA YAFIKIA MILIONI 10

Ofisi ya sensa ya Rwanda imetoa ripoti ikisema, hadi kufikia mwaka 2011 idadi ya watu nchini Rwanda imefikia milioni 10.7, na wanawake nchini humo wanachukua 52%. 

Ripoti hiyo inasema katika takwimu hizo idadi ya watu wenye umri kati ya miaka 15 hadi 59 ni wengi zaidi na kuchukua 53.8% ya idadi ya jumla ya watu wa Rwanda.
Ofisi hiyo imesema Rwanda ni nchi yenye ongezeko kubwa la idadi ya watu barani Afrika, na idadi hiyo inaongezeka maradufu kila baada ya miaka 25.

No comments:

Post a Comment