Sunday, July 3, 2011

SERIKALI YASHAURIWA KUJENGA MIUNDOMBINU RORYA

KANISA la Menonite  Tanzania KMT, Doyosisi ya Mara kaskazini,limeishauri Serikali kujenga miundo mbinu itakayowezesha maji ya ziwa Victoria kutumika kwaajili ya kilimo cha umwagiliaji ikiwa ni njia moja wapo ya kukabiliana na ukame.

Kauli hiyo imetolewa na askofu wa kanisa hilo Dayosisi ya Mara kaskazini John Nyagwegwe,wakati akizungumza katika warsha ya wadau wa maendeleo wa wilaya ya Rorya ya uandaaji wa mpango mkakati wa halmashauri ya wilaya hiyo.

Amesema vijiji vya kata 13 kati ya 21 vya wilaya ya Rorya,viko pembeni mwa ziwa Victoria lakini wananchi wameshindwa kutumia maji yake kwa ajili ya kilimo hicho kutokana na ukosefu wa miundombinu muhimu  ya umwagiliaji.

Hata hivyo askofu huyo wa KMT,amesema umefika wakati kwa serikali kutafuta nja ya haraka ya kukabiliana na ongezeko la ajira kwa vijana wanamaliza elimu ya sekondari  kwa kuanza kuongeza kasi ya ujenzi wa vyuo vya ufundi ambavyo vitasadia vijana wengi kupata ujuzi na kujiajiri wenyewe.

No comments:

Post a Comment