Sunday, July 3, 2011

NJAA KALI KUIKUMBA SERENGETI


Zaidi ya kaya 150 katika vijiji vitatu vinavyozunguka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ziko zinakabiliwa na njaa kali iliyosababishwa na tembo wanaoharibu mazao ya chakula Wilayani Serengeti mkoa wa Mara.

Diwani wa kata ya Sedeko  Richard Nyakera alithibithisha  kwa waandishi wa habari mjini Mugumu juzi kuwa njaa imieishapisha hodi katika vijiji vitatu  vya kata hiyo baada ya  kwa sababu ya tembo,Alivitaja vijiji hivyo kuwa ni Bisarara, Mbirikiri na Bhonchugu.

“ Zaidi ya kaya 150 zina hali mbaya  na mpaka sasa kuna makundi ya tembo  huko vijijini na wameharibu kila kitu”, alilalamika  diwani Nyakera.

Kwa mujibu wa Nyakera  tayari walishapeka taarifa  kwa ofisi ya mkurugenzi wa  wa halmashuri ya wilaya ya Serengeti  kuhusiana na uharibifu huo.

“Tembo walianza kaharibu mazao yam tama, mahindi na mihogo kuanzia mwezi wa tano hadi sasa wanaendelea”  aliongeza Nyakera.

Wakati huo huo maafisa wa idara ya wanyama pori halmashauri ya wilaya ya Serengeti wamemuua tembo mmoja katika kijiji cha Kitarungu baadaya kutishia maisha ya wananchi.

“Tulikuwa hatuna jinsi ya kufanya, bali kumuua kwa kumpiga risasi tembo yule ili kunusuru maisha ya wananchi” alisema kaimu ofisa wa wanyamapori katika halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Catthbert Boma.

Tatizo la uvamizi wa tembo katika vijiji vinavyozunguka Hifadhi  ya Serengeti limeendelea kuwatesa  sehemu kubwa  ya wananchi wanaoishi chini ya dola moja siku.

Hata hivyo TANAPA inalaumiwa kwa kupuuza tatizo la tembo   linalowakabili  wananchi wanoaishi jirani na hifadhi za taifa nchini.

Habari hii ni kwa mujibu  wa Waitara Meng’anyi, kutoka Serengeti mkoani Mara

No comments:

Post a Comment