Sunday, June 19, 2011

MAUJI YA TARIME YAOMBWA KUCHUNGUZWA

MUSOMA
 
CHAMA cha wataalamu wa ustawi wa jamii mkoani Mara (TASWA) wamelaani vikali mauaji yanayotokea wilayani Tarime katika eneo la Nyamongo mkoani hapa na pia wakiiomba serikali kufanya uchunguzi na kubaini chanzo cha mauaji hayo pamoja na kuyatolea maamuzi 

 
Kauli za wataalamu hao zimetolewa jana wakati Wataalamu hao wakichagua viongozi wa mkoa wa chama hicho  na kujiwekea mikakati ya kufanya kazi ya taaluma yao bila kushinikizwa na taasisi yoyote.

 
Akisoma risala ya chama hiyo mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Mara Iddi Mtani alisema kuwa ni wajibu wa wataalamu wa ustawi wa jamii kufanya uchunguzi ili kubaini ni kwanini mauaji hayo yalitokea ili waliohusika wafikishwe kwenye vyombo vya sheria. 

 
Mwenyekiti huyo alisema kuwa mauaji hayo yawezekana yakawa na chimbuko lake kitu ambacho kama uchunguzi utafanyika kutaweza kubaini  chanzo cha mauaji hayo.
“ Yawezekana hapa kuna kitu ambacho kimejificha na tunaimani kama utafiti utafanyika bila shaka chanzo cha mauaji hayo yatabainika” alisema mwenyekiti huyo

 
Mbali na kauli hiyo mwenyekiti huyo aliiomba serikali kuingilia suala hilo ili kuondoa mgongano  uliopo dhidi ya majukumu yanayotakiwa kutekelezwa na ustawi wa jamii pamoja na yale yanayotakiwa kwa upande wa maendeleo ya jamii.
Alisema kuwa mara nyingi kazi zinazotakiwa kutekelezwa na ustawi wa jamii zimekuwa zikifanywa na idara ya maendeleo ya jamii swala ambalo alisema limechangia kazi hizo kutofika mwisho na wakati mwingine kuisha bila kupata majibu ya kurizisha au mafanikio.

 
Naye mgeni rasmi katika mkutano huo Clement Lujaji alikiri kuwepo kwa mauaji hayo ambayo alisema kuwa  yanatishia amani  ya mkoa wa Mara ikiwa ni pamoja na kushindwa kuthamini mchango wa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere katika kudumisha umoja na Amani hapa nchini.

 
Mgeni rasmi huyo alisema kuwa mkoa wa Mara ulitakiwa kuwa kivutio  kwa watu wa mikoa mingine kwa lengo la kutaka kufahamu historia ya Baba wa Taifa lakini badala yake mkoa umekuwa na matukio yanayosikitisha.

 
Aidha Katibu tawala huyo alisema kuwa atakuwa na wataalamu hao katika kuhakikisha uchunguzi huo unafanyika ili kubaini chanzo na mauaji hayo na mapendekezo juu ya tukio hilo.

 
 MWISHO

No comments:

Post a Comment