Friday, January 7, 2011

ZIARA YA WAANDISHI WA HABARI WA MKOA WA MARA KATIKA HIFADHI YA NGORONGORO

  Waandishi wa habari kutoka mkoani Mara wakiwa ndani ya bonde la Ngorongoro wakifanya mahojiano na mhifadhi msaidizi Abdel kuhusu mambo mbalimbali katika bonde hilo
Ziara ilikuwa ni kubwa katika hifadhi hiyo ya Ngorongoro na hapa nilibahatika kukutana na afisa mahusiano katika hifadhi hiyo Adam Akyo na kumjulisha juu ya blog yangu ili tuone ni jinsi gani blog hii inaweza kutumika katika kuitangaza hifadhi hiyo
Katika mkutano na waandishi wa habari wakuu wa idara mbalimbali walikuwepo katika kutoa ufafanuzi katika hifadhi hiyo kama wanavyoonekana katika picha
Hili ni basi ambalo linatumika katika kusafirisha watalii wa ndani na nje kuwapeleka katika Bonde la Ngorongoro ambapo hata hivyo mhifadhi mkuu wa hifadhi hiyo Bernad Mrunya alisema kuwa litatumika kusafirisha watalii wa ndani kutoka jijini Arusha na baadaye mikoa ya kanda ya ziwa.jamani tuamke
 Shomar binda mtangazaji wa Victoria Fm alikuwepo katika ziara hiyo na hapo anaonekana akiwa amepozi kwambali unamuona Twiga
                                       Abdel akiendelea na mahojiano
 Huyu ni mkuu wa kitengo cha maendelo ya Jamii katika hifadhi hiyo Dr Justice na hapa alikuwa akitoa ufafanuzi
                                     Picha ya Kiboko akiwa majini
Mwandishi wa habari wa ITV mkoani Mara George Marato nae aalikuwepo katika ziara hiyo ya siku tatu
 Mwana wa Afrika akifurahia kuona rasilimali ya nchi ilivyo,wanyama kama hawa wapo kwetu jamani
                                          Baada ya kazi mapumiziko
Afisa uhusiano katika hifadhi ya Ngorngoro Vincent akibadilishana mawazo na waandishiwa wa habari
Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya Ngorongoro Bernad Mrunya akiongea na waandishi wa habari waliotembelea hifadhi hiyo hivi karibuni
                                                   Bernad Mrunya
          Ndege anayesadikika kuwa na kilo nyingi zaidi ya wote,kilo 12
                Hawa ni ndege wanaohama kutoka nchi moja kwenda nyingine kulingana na hali ya hewa
                                   Sura nzuri ya bonde la Ngorongoro
            Paschal Michael mmoja wa waandishi wa habari mjini Musoma akiwa katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro
                                   Simba akiwa amepumzika katika bonde la Ngorongoro

       Kiongozi wa msafara wa waandishi wa habari kutoka mkoani Mara Maximilian Ngessi akifafanua jambo kwa mhifadhi mkuu
Mpenzi mtazamaji wa blog hii habari ni nyingi sana ambazo tumezipata kutoka katika bonde la Ngorongoro hivyo nitakuwa nakuletea siku hadi siku

No comments:

Post a Comment