Friday, January 7, 2011

MRPC WANENA VURUGU ZA ARUSHA


     Wananchi wa manispaa ya Musoma wakifuatilia habari katika kibanda cha kuuzia magazeti mjini hapa leo Asubuhi


Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mara MRPC kimelaani vikali kitendo cha askari wa jeshi la polisi mkoani Arusha kuwakamata,kuwapiga na kuwanyang’anya vitendea kazi vya baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa arusha wakati wakiwa kazini.
Waandishi walipigwa wakati wakiwa katika shughuli zao za kawaida katika kuandika habari za maandamano yalioitoishwa na chama cha Demokrosia na maendeleo CHADEMA ni  Ashraf Bakari ambaye ni mpiga picha wa kituo cha Channel Ten,Moses Kilinga wa shirika la utangazaji la Uingereza BBC,Moses Mashala wa gazeti la Mwananchi ambapo pia Musa Juma wa Mwananchi na Kilinga walikamatwa baadaye na kuachiwa usiku.
Katibu wa MRPC Emanuel Bwimbo,katika mazungumzo yake na waandishi wa habari mjini Musoma wakati akitoa tamko la chama hicho,alisema kutokana na polisi kushindwa kujua wajibu wao wa kazi kwa kuwazuia wanahabari hao kutimiza wajibu wao kwa umma kwa mujibu wa katiba ni vema waziri wa mambo ya ndani ya nchi na mkuu wa jeshi la polisi nchini wakaweka mbele maslahi ya taifa kwa kuachia ngazi.
“Nchi hii ni yetu sote na kila raia ana haki sawa sasa kitendo kilichofanywa na polisi hawa kwa kuwanyima haki wanahari hao kutekeleza wajibu wao ni ukiukwaji mkubwa wa katiba hivyo ni jambo la busara tu kwa mtu mzima kama IGP Mwema na waziri wake wakaachia ngazi,kwanza kwa kitendo hicho pili kwa kushindwa kulinda amani mjini arusha badala yake kuwa chanzo cha machafuko”alisema Bwimbo.
Bwimbo alisema polisi walio wengi wamekuwa wakifanya kazi yao pasipozingatia sheria na haki za wananchi kutokana tu na kutekeleza maagizo ya wakubwa wao ambayo mengine mara nyingi yamekuwa hayana maana jambo ambalo sasa linakiweka chombo hicho cha kusimamia usalama sehemu mbaya ya kutoheshimika katika jamii.
Hata hivyo kiongozi huyo wa MRPC alitaka jeshi la polisi kuhakikisha linatoa fidia kwa waandishi hao, matibabu na kurudisha picha na vifaa vyao vya kazi vinavyodaiwa kuchukuliwa muda mfupi baada ya kuwakamata.
Kwa mujibu wa Bwimbo,waandishi hao wa habari walipatwa na mkasa huo juzi kwa nyakati tofauti jijini arusha wakati wakitekeleza majukumu yao katika maandamano yalioitishwa na Chadema kupinga uchaguzi wa Meya wa jiji la arusha.

No comments:

Post a Comment