Tuesday, January 18, 2011

VIJANA WA CCM MARA WANENA JUU YA DOWANS


WAJUMBE wa baraza kuu la umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mara wamekitaka chama kilichoshika dola kuitaka Serikali kutamka kuwa kampuni ya kufua umeme ya Dowans kuwa ni kampuni hewa na ambayo kamwe hastahili kulipwa kiasi chochote cha fedha za walipa kodi wa Tanzania wa lio masikini. 

Kauli hiyo imetolewa katika  mkutano ulioitishwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara kupitia vijana Esther Bulaya ikiwa ni njia ya kuwashurua wajumbe mkutano uliofanyika katika  ukumbi wa CCM mkoani hapa, Katika mkutano huo wajumbe hao walisema endapo Bunge la jamhuri ya muungano lilibaini wazi kuwa kampuni ya kufua umeme ya Richmond ni kampuni hewa iweje leo Dowans iliyorithi mikoba yake ikawa ni kampuni halali ya kulipwa fedha hizo. 

Wamesema  ukimya kwa chama hicho wakati serikali yake ikiendelea na mchakato wa kuilipa Dowans kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 94 itatafasiliwa wazi kuwa kinahusika moja kwa moja na njama hizo za wizi wa fedha za umma ambapo atalipwa mtu asiyefahamika

Katika mkutano huo mjumbe wa baraza la umoja wa vijana wa CCM mkoa wa Mara Fidelis Manyerere alisema kuwa umefika wakati Vijana wa CCM kuwa wa kwanza katika kutetea masilahi ya Taifa,mbunge huyo aliongeza kuwa leo Dowans inapataje uhalali wa kulipwa ile hali Kampuni ya Richmond tulielezwa kuwa ni kampuni hewa.
Aliongeza kuwa  ili kulinda heshima ya Chama hicho ambacho kimejengwa kwa miaka mingi lazima viongozi wakuu wakaishauri serikali kuacha kulipa kampuni hiyo huku akitahadhalisha kuwa endapo fedha hizo zitalipwa kwa dowans chama hicho kitakuwa katika wakati mgumu hasa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015. 

Mjumbe huyo pia alishauri ccm kuacha kutoa taarifa kwa wananchi zinazopingana kila wakati jambo ambalo limekuwa likitafsiliwa kwa wananchi kuwa sawa na gulio. 

“ Chama chetu cha CCM sasa kila mtu amekuwa ni msemaji leo utamkuta Mkuchika na hili,kidogo unasikia kwa Chiligati,akitoka unamsikia Makamba mara Tambwe Hiza sasa huu si utaratibu mzuri nadhani tusifanye chama kama gulio ambalo kila mtu akiingia anasema atakavyo”alisisitiza mjumbe huyo.
Aidha mjumbe  kutoka wilaya ya Tarime ambaye kwa sasa anakaimu nafasi ya katibu msaidizi wa wilaya ya Tarime Denis Zacharia alisema  suala la katiba bado ni tatizo na inasikitisha kwa kiasi kikubwa kwa chama hicho kutozungumzia suala hilo wakati wakitambua wazi hoja hiyo ni ya taifa nzima kwa sasa. 

Alisema kwa sasa wana CCM wameanza kuogopa makongamano na kutokana na uoga huo umesababisha hivi vijana wa ccm kukosa uthubutu hata wa kuhutubia ama kuelezea mafanio ya serikali katika mikusanyiko ya watu jambo ambalo ni hatari kwa chama cha mapinduzi. 

Kwa upande wa mwenyekiti wa UV-CCM mkoa wa Mara Marwa Mathayo alisema wakati umefika kwa vijana kujipanga vizuri kwa kuwashauri viongozi wa ccm kuibana serikali yake kutekeleza mambo mbalimbali yanawakabili wananchi ili kuepuka kuhojiwa wakati wa chaguzi jambo ambalo limekuwa likisababisha kuangushwa na wapinzani katika kata,majimbo hata kupunguza kura za rais.,alisema vijana waepuke kutumiwa na wanasiasa kwani kwa kufanya hivyo Taifa litaangamia.

   ”Vijana tuepuke kutumiwa maana sisi ndio tunatakiwa kukijenga Chama sasa kama tutakuwa watu wa kutumiwa chama kitafika wapi” alihoji mwenyekiti huyo

Sakata la Dowans na Katiba limechukua sura mpya nchini baada ya wadau wa siasa na elimu kuanzisha mijadala mbalimbali kuhusu masuala hayo

No comments:

Post a Comment