Tuliamua kuvuka mpaka tukaingia sehemu ya nchi ya Kenya ili kuona wenzetu wanaishi vipi
Bado tuko sehemu ya pili ya Mpaka yaani nchini Kenya
Hatukuwa na gari tuliamu kupaki gari na kuanza kutembea kwa miguu kama ujuavyo kwa kufanya hivyo tuliweza kuona mengi
Moja ya mambo ambayo tuliyaona ni kama hivi,sio kwetu Tanzania tu ndio watu hawazingatii suala la usafi hata nchi ya Jirani(Kenya) hali ni hiyo hiyo
Katika hotel hii tulifika japo kupata kinywaji lakini hatukuweza kupata kutokana na sheria ya Kenya kuwa hawaruhusiwi kuuza wakati wa kazi mpaka majira ya saa kumi na moja jioni
Kesho yake tulianza safari ya kwenda maeneo ambayo huwa kuna mapigano ya Mara kwa Mara mjini Tarime,hii ni shule ya Kubiterere ambapo inasemekana hapo ndipo kuna uwanja wa mapigao wa koo zinazopigana mara kwa mara wilayani humo
Shule zingine zahitaji moyo kupata elimu bora
Huyu ni mmoja wa walimu katika shule hiyo na hapa alikuwa akitupatia historia kuhusu mapigano ya huko na nini kifanyike ili mapigano haya yaishe
Huu ndio uwanja wa mapigano
Uwanja wa mapigano jamani
Baada ya hapo tuliingia mpaka shule ya sekondari Mwema na kukuitana na walimu wa shule hiyo ambao pia walitueleza kuwa shule hiyo ipo kwenye mpaka ambao wapiganaji hujipanga na kuanza kurushiana mishale
Maelezo yanaendelea
Baada ya walimu nilikutana na huyu mzee ambaye ni mwenyeji wa eneo hilo ambapo pia alitueleza kiini cha mapigano
Mdau kuna sehemu mawasiliano mpaka utumie mbinu mbadala hili upate mawasiliano
Baada ya shule ya Mwema tulifika katika kijiji cha Susuni na kukutana na mtanzania huyu ambaye anasema aliwahi kushiriki mara mbili mapigano hayo
Huyu babu alimpoteza mke wake ambaye aliuawa katika mapigano ya mwisho
Pamoja na yote lakini mwanamke kuchunga Ng'ombe katika jamii ya wakurya ni jambo la kawaida sana
Kazi inaendelea hapa,lakini kipindi namuomba mama huyo nimpige picha ili nitumie kwenye blog yangu alinihisi kuwa natokea jamii ya Walyanchoka na kumpiga picha ni kama vile nataka kuiba ng'ombe hizo ila baada ya maongezi ya takriban dk 3 tulielewana na kukubali kupigwa picha
Hali ya Tarime kwa Kilimo ni bomba ile mbaya kwanini watu wasiwekeze kwenye kilimo?
Baada ya ziara yetu ya mafanikio tuliamua kurudi home,na hapa Sefroza Joseph ambaye alikuwa amenipa shavu kwenye gari yake akiwa amepozi baada ya kuchoka kuendeshaBinti yupo kamini barabarani ila ............................................
Mdau hibvi karibuni nilikuwa wilayani Tarime maeneo ya Sirari ambapo huwa kuna mapigano ya koo mbalimbali za jamii ya wakurya,kuna mengi ambayo waliongea kuhusu mapigano hao.
Taarifa zaidi mdau kuhusu nini walichokiongea nitakuandika baadaye ili uweze kujua kwanini mapigano hayo huwa hayaishi?
No comments:
Post a Comment