Tuesday, January 11, 2011

HUU NDIO MCHANGA UNAOHAMA NGORONGORO

Mtazamaji wa blog ya mwana wa Afrika picha hizi ni mwendelezo wa ziara ya waandishi wa habari kutoka mkoani Mara katika hifadhi ya Ngorongoro na huu n i mchanga ambao wataalam wa mambo ya makumbusho wanasema kuwa unahama kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.Ni mchanga laini ambao utatamani kuushika muda wote.

Pamoja na hivyo pia katika eneo hilo la makumbukusho nilielezwa kuwa kuna mjerumani ambaye alipotosha jina la Oldupai Gorge na badala yake kwa kushindwa kutamka neno hilo alisema kuwa olduvai gorge

Mtanzania kuwa wa kwanza kutembelea makumbusho katika nchi yako, na si mgeni ndiye akusimlie hapo vip?

No comments:

Post a Comment