Saturday, January 8, 2011

CHALLENGE MUSOMA CHANGE.

ALIYEKUWA mgombea ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) katika kura za maoni Eliud Esseko Tongola almaarufu kwa jina la Mkorea amesema kamwe hatosita kusaidia watu wa Musoma hata kama kura za yeye kuteuliwa kuwa mbunge hazikufika.

Kauli hiyo ameitoa leo mjini Musoma wakati akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa  hotel ya Orange Tree ambapo alisema kuwa kiongozi bora anapimwa kwa vitendo na si maneno kwani wananchi hawaitaji maneno.

Tongola ambaye alionekana kukubarika  vyema kwa rika mbalimbali mjini Musoma katika kinyang’anyiro hicho cha kura za maoni alisema kuwa pamoja na kujitoa katika kuwasaidia watu wa Musoma lakini aliwashukuru kwa kuendesha vyema uchaguzi mkuu na kuwachagua viongozi waliowataka.
Alisema kwa sasa ataanza kutekeleza ahadi ambazo aliziahidi wakati wa kampeni za kura za maoni ndani ya CCM ili kuleta maendeleo kwa watu wa Musoma,Tongola aliongeza kuwa lazima Musoma ijengwe na wanamusoma na si kusubiri mpaka bunge liamua ndipo Musoma ijengwe.

Pamoja na kutoa shukrani kwa watu wa Musoma na kuahidi kutekeleza ahadi ambazo aliziahidi,Tongola alisema kuwa kwa kuanza atanza kwa kuisaidia Hospital ya Mkoa vifaa ambazo anaamini vitakuwa msaada mkubwa kwa watumishi wa hospital hiyo ili huduma bora ipatikane kwa wananchi.

Alisema kuwa mashine atakazozileta katika hospital hiyo zitakuwa tatu ambapo kila moja inathamni ya dola 460,aliongeza kuwa ni aibu katika hospital kama hiyo mtu kufua kwa mikono kwani kufanya hivyo kunaweza kupelekea magonjwa mbalimbali.

Aidha Mtanzania huyo anayeishi Korea Kusini alisema kuwa pamoja na kusaidia Hospital hiyo lakini kamwe hatoisahau shule ya secondary Mara ambapo ndipo alipata elimu yake ya Sekondary hivyo ameona ni bora akatoa msaada wa mitambo ya gesi katika jiko la shule hiyo ili kusaidia kupunguza matumizi mabaya ya miti katika nchi yetu.

Tongola alisema kuwa mitambo hiyo ya gesi itagharimu kiasi cha dola za kimarekani 582 kitu ambacho anaimnai kitakuwa msaada mkubwa kwa shule hiyo.

Katika mlolongo huo Tongola alisema kuwa jambo la tatu ambalo atapambana nalo ni kusaidia vikundi vya kijasiriamali ambavyo tayari vimeonesha nia ya kusaidiwa na kuongeza kuwa atahakikisha vikundi vyote vinasajiliwa ambapo atamtafuta mwansheria na kumlipa ili asaidie vikundi hivyo.
Mbali na kuelezea malengo hayo kwa watu wa Musoma Tongola ama kwa jina Maarufu mjini hapa Mkorea alisema kuwa tayari amekwisha watafutia shule watunwatatu kutoka Musoma na mwezi February wataelekea Korea Kusini katika suala zima la masomo.

Aliongeza kuwa mbali na watu hao lakini pia kuna watu wengi wane ambao wanaweza kwenda kozi fupi nchini humo ili kuongeza maarifa ili warudi katika kuisaidia Musoma ipate mabadiliko ya Kweli

Tongoala alimaliza kwa kusema kufanya hivyo ni kuonyesha jinsi gani amedhamiria mji  wa Musoma kuwa katika mabadiliko na isiwepo dhana ya kudhani kwamba alikuja kutafuta uongozi ili arudi korea kusini kukaa,aliongeza kuwa kama wanamusoma wataamua basi Musoma itabadilika huku alimalizia kwa kusema CHALLENGE MUSOMA CHANGE

No comments:

Post a Comment