Hili ni moja ya jengo ambalo limefadhiliwa na TASAF lakini kwa sasa limeonekana kuchakaa kutokana ni ujenzi kuwa chini ya kiwango
Meya wa Manispaa ya Musoma Alex Kisurura akitazama sakafu iliyovunjwa na wanakamati wakidai eti ni mbovu baada ya kuletewa fedha zingine za kukamilishia jengo
Wajumbe waliokuwa katika ziara hiyo wakiangalia ratiba kabla ya kuanza ukaguzi
Mratibu wa mfuko wa TASAF Bi Grace Muniko akiwa na injinia wa Manispaa katika ziara hiyo
Bi Grace Muniko
Mmoja wa wenyeviti katika kamati za ujenzi akifafanua jambo kwa viongoiz wa halmashauri
Injinia akitoa ufafanuzi
Injinia akitoa ufafanuzi
Injinia akiwa amepozi baada ya ufafnuzi
Meya Alex Kisurura akitazama sakafu iliyotolewa wakidai mbovu
TASF
Meya wa Musoma Alex Kisurura na Bi Grace Muniko
Tazama jengo la serikali mbao zinazotumika
Mhe Mbunge wa Musoma mjini Vincent Nyerere akitoa ufafanuzi
Vijana hawakuwa nyuma katika kuhakikisha kama kweli watu wanawekwa kiti moto
Ufafanuzi
Kifaa cha maabara kikiwa chini yaani zahanati haina meza na mh Mbunge aliahidi kuwapelekea meza
Mh Mbunge Nyerere akitazama chumba cha uzazi
Wazee hawa walimtafuta mbunge kumpatia hongera ya ushindi
Jamani ndio elimu yetu hakuna sakafu fedha watu wamekula
Diwani wa Iringo kulia akieleza ujumbe huo kuwa hana taarifa juu ya uakaguzi huo na aligoma kutoa ushirikiano
Miradi inayotolewa na TASF imeonekana kuwanufaisha wachache katika manispaa ya Musoma mkoani Mara baada ya ziara iliyofanywa na mbunge wa jimbo la Musoma Vincent Nyerere na Meya wa manispaa hiyo Alex Kisurura.
Katika ziara hiyo tulishuhudia baadhi ya miradi iliyotolewa na mfuko huo katika awamu ya kwanza ilikuwa imebomolewa huku wenyeviti wa kamti za ujenzi wakijiandaa kurudia eneo hilo tena katika kujenga
Katika hali hiyo Mbunge wa jimbo La Musoma alisema kuwa inashangaza kuona watu wachache ambao wamepewa dhamana ya kusimamia mali ya umma wanafanya mambo ambayo hayafai.
Naye Meya wa Manispaa ya Musoma alisema kuwa katika kipindi hiki cha uongozi wake atajitahidi kila fedha inayotolewa na wafadhili inasimamiwa kama ilivyokusudiwa
Aidha katika ziara hiyo kitu cha kushangaza ni pale ambapo diwani wa kata ya Iringo aligoma kupokea ujumbe huo akidai kuwa hana taarifa
No comments:
Post a Comment