Friday, December 31, 2010

NYAMBARI NYANGWINE AWAPONGEZA WAKAZI WA TARIME

                                Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tarime
                                                Mchungaji
                                               Shehe akitoa dua
                                            Mwakilishi toka serikalini
    Aliwahi kuwa mbunge wa jimb o la Tarime lakini kwasasa ni mbunge wa jimbo la Babati anaitwa Mh Chambiri
                                       Hapo je?
                                                Mkuu wa wilaya ya Tarime
                             Mama Gaudencia Kabaka waziri wa kazi na ajira
      Mh Stiven Wassira mbunge wa jimbo la Bunda na waziri katika serikali ya Muungano
                                     Mbunge wa jimbo la Tarime Nyambari Nyangwine


                                                          BURUDANI KAMA KAWA

                                                        Mh Nyangwine
                                                 Uzalendo uliwashinda
                                            Umati wa watu waliokuwepo katika sherhe hiyo

                                     
                                                   CHIEF MAKER ALITOA BURUDAN

Duuh kazi ilikuwa pevu      

MBUNGE wa jimbo la Tarime mkoani Mara Mh Nyambari Nyangwene ameahidi kutoa vitabu vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 320 kwa shule 32 za Sekondari za jimbo hilo la Tarime.
Mh Nyangwine alisema hayo mjini Tarime wakati akiongea na waandishi wa habari ambapo mpango huo utaanza kutekelezwa mwezi januari ambapo kila shule ya Sekondari ya jimbo hilo itapata mgao wa vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni 10.
Alisema kuwa vitabu hivyo ambavyo vitatolewa na makampuni za uchapishaji za Nyambari Nyangwine Pulishers,vitasadia kupunguza tatizo kubwa la upungufu wa vitabu linalozikabili shule hizo za Sekondari wilayani Tarime.
Hata hivyo Mh Nyangwine,alisema tayari ameanza mchakato wa ujenzi wa chuo kikuu cha elimu ya ufundi VETA wilayani Tarime ambacho kitasadia vijana wengi kujiunga na chuo hicho na baada ya kuhitimu wataweza kujiajiri ikiwa ni njia moja wapo ya kupambana na tatizo la ajira kwa vijana.
 Pamoja na hivyo pia Nyangwine alisema kuwa ili kuondoa kero ya watoto wasiokuwa na ajira katika kipindi cha miaka mitano atajenga chuo cha VETA ambapo maandalizi yake yanaendelea vizuri na kuhakikisha umeme unasambaa vijijini 

No comments:

Post a Comment