Wednesday, December 8, 2010

MHESHIMIWA NYERERE ASIMAMISHA UJENZI WA SEKONDARY

        Hili ni ndilo jengo la Sekondary ya Nyasho ambalo Mheshimiwa Nyerere amesimamisha ujenzi wake baada ya mkandarasi ambaye ni mtendaji wa kata ya Nyasho kuchukua tender hiyo na kuipeleka kinyume na taratibu katika hali ya kuchakachua fedha za umma
       Mheshimiwa Nyerere akipewa maagizo ya kitaalamu yanayotakiwa yafanyike katika ujenzi wa jengo hasa hilo la sekondary ambalo linajengwa kwa udongo na mkandarasi ambaye ni  mtendaji wa kata ya Nyasho
    Unapokuwa kiongozi usikubari kuficha maovu kama anavyoonekana Mbunge Nyerere akitoa maelezo katika jengo hilo ambalo liko chini ya kiwango  cha majengo ya sekondary nchini
 Mheshimiwa Nyerere akimwagiza mtendaji wa kata ya Nyasho (Mkandarsi) Everist Tiginga kuhusu ubovu wa jengo hilo ambalo fedha zilizotoka ni za kukamilishia majengo mawili lakini hapo limeonekena moja huku fedha yote akidai imetumika hapo kweli jamaaaaaaaaaaaaaaaaaaani
          Mheshimiwa Nyerere akielezwa jambo na Msaidizi wake
                           Baada ya kauli sasa ni utekelezaji
              Ukuta ambao umeonekana kutokuwa na kiwango
  Katika bajeti ya kamati ya Kata imeonyesha kuwa kutakuwa na trip moja ya mchanga lakini cha ajabu tulikuta watu hawa wakiwa nasomba mchanga kama unavyowaona
                               Hii ndio trip ya mchanga katika lori?
      Jengo mojawapo katika shule hiyo ambalo hata mwaka halijamaliza tayari limebomoka
       Mtendaji wa kata ya Nyasho (Mkandarasi) Everist Tiginga

 Safari ya kutazama document za ujenzi huo katika ofisi ya mtendaji huyo ilianza  hiyo ndio ofisi ya kata ya Nyasho
   Utambulisho muhimu,mheshimiwa akiweka sahihi katika ofissi hiyo
  Mheshimiwa akitazama stakabadhi ambazo gharama zake ni tofauti na gharama zilizoandikwa kwenye bajeti
                Mheshimiwa Nyerere akisistiza jambo ofisini hapo
    Wananchi wa Nyasho hawakuwa nyuma kuongea na mbunge wao

AGIZO

Mbunge wa jimbo la Musoma mjni Mheshimiwa Vincent Nyerere amesimamisha ujenzi wa shule ya secondary ya Nyasho baada ya ujenzi huo kuendeshwa bila mtaalamu ambapo umepelekea ujenzi wa jengo  hilo ukiwa chini ya kiwango.

Amesema kuendelea kuruhusu kujengwa kwa darasa la shule hiyo ni kukaribisha maafa ambayo yanaweza kutokea kwa wanafunzi watakaolitumia jengo hilo huku watu wachache wakiendelea kunufaika kwa udanganyifu wanaoufanya katika ujenzi

Mhesimiwa Nyerere ambaye alikuwa amefuatana na kamati yake ya kutembelea shule mbalimbali za jimbo la Musoma amesema kuwa anataarifa kuwa shule hiyo imepewa kiasi cha shilingi milioni 4 kwa majengo mawili lakini katika shule hiyo ni jengo moja linaloonekana.

Aidha kufuatia hatua hiyo mheshimiwa Nyerere amemwagiza mtendaji wa kata ya Nyasho Everist Tiginga kuhakikisha shilingi milioni mbili zilizosalia zinapatikana ili zitumike katika kutengeneza madawati ili mwanafunzi yeyote atakayejiunga na shule hiyo hasiweze kulipa gharama za madawati.

Ujenzi wa jengo hilo la darasa ambao umekuwa ukisimamiwa na mtendaji wa kata hiyo umeendeshwa bila kuwepo na mtaalam yeyote wa majengo kutoka katika halmashauri ya manispaa ya Musoma  huku wahusika wakisema kuwa hawajui kinachoendelea juu ya ujenzi huo.

Baada ya kutakiwa kuelezwa kwa kina nini ambacho kinaendelea katika ujenzi huo mtendaji huyo ambaye muda wote alionekana kubabaika alisema kuwa ujenzi huo amehusishwa diwani wa kata hiyo Godwin Mumbala ambaye hata hivyo alipotafutwa na mheshimiwa mbunge kwa njia ya simu alikiri kufahamu kuwepo kwa kikao hicho lakini hajahusishwa katika suala zima la bajeti ya jengo hilo.

Mbali na kuwepo kwa majibu yasiyoendana na ukweli kutoka kwa mtendaji huyo wa kata ya Nyasho kwa mheshimiwa mbunge ndipo safari ya kuelekea katika ofisi yake ilipoanza ili kubaini kile ambacho alikuwa akikieleza katika eneo la jengo hilo.

Katika ofisi ya mtendaji huyo baada ya kutoa karatasi mbalimbali ambazo zilikuwa zikionyesha bajeti nzima ya jengo hilo na stakabadhi za manunuzi ndipo mheshimiwa mbunge alipogundua kuwepo utofauti wa gharama za manunuzi na zile zilizoandikwa katika bajeti ya kamati ya mtendaji huyo.

Kufuatia kuwepo kwa utofauti huo mheshimiwa Nyerere amesema kuwa atahakikisha mtendaji huyo anarudisha kiasi cha fedha zilizosalia katika ujenzi huo lakini pia ahakikishe ujenzi ambao utaendelea katika jengo la shule hiyo unakuwa wa kiwango tofauti na ulivvyo sasa ambapo mtendaji huyo aliyebadilika kuwa mkandarasi anaufanya
No comments:

Post a Comment