Wednesday, December 8, 2010

MBUNGE JIMBO LA MUSOMA MJINI ATEMBELEA VICTORIA FM LEO

 Mbunge wa jimbo la Musoma mjini Mheshimiwa Vincent Nyerere leo ametembelea kituo cha redio cha Victoria fm cha mjini Musoma ambapo alikutana na meneja wa kituo hicho John Katute kulia ambapo aliongea na wananchi wa jimbo hilo kuhusu mikakati ya kuleta maendeleo jimboni humo
        Mheshimiwa Nyerere akijibu moja ya swali aliloulizwea na mtangazaji wa kituo hicho Cares one juu ya mikakati katika kutatua suala la maji katika jimbo la Musoma mjini hasa kwa wale ambao miundombinu ni migumu kupitisha mambomba,katika swali hilo mheshimiwa Nyrere amesema kuwa atakikisha katika maeneo kama hayo kunakuwepo na visima vya maji vilivyochimbwa kisasa wakati suala la mabomba likishughulikiwa
 Mtangazaji wa Victoria fm Sefroza Joseph ama Self wa Ukweli naye alitaka kuuza akiwa karibu na mbunge Nyerere studioni hapo
 Meneja wa Victoria Fm akishukuru ujio wa mbunge huyo katika kituo hicho na kuahidi kushirikiana kwa ukaribu katika suala zima la kuleta maendeleo jimboni humo
 Mtangazaji wa redio hiyo Cares one akimuuliza mbunge swali juu ya majini katika jimbo la Musoma mjni
Sikutaka kubaki nyuma hasa kuhusu suala zima la vibanda katika kituo kikuu cha mabasi cha mjini Musoma maana kuwa baadhi ya watu ambao wanavibanda viwili na kuendelea huku walengwa wakiwa hawana chao,Mheshimiwa Nyerere amesema kuwa baada ya kuapishwa kwa madiwani Decemba 17 mwaka huu watapitia mikataba yote na kuangalia kwa ukaribu suala hilo

No comments:

Post a Comment