Wednesday, November 10, 2010

NI KWELI AU ALIKUWA ANAZUGA?

  Mwenyekiti wa CCJ enzi hizo Richard Kyabo akilia katika kaburi la Baba wa Taifa Butiama,aliongea mambo mengi sana kuhusiana na Chama cha Mapinduzi lakini baada ya kugonga mwamba katika usajili alikimbilia CHADEMA na baada ya kuona kule wajanja wengi akakimbilia  NRA na kuchukua fomu za kugombea nafasi ya urais huku akisema dunia leo ni kama kijiji baada ya kuulizwa na waandishi kama ataweza kutafuta wafadhili. Hatujaakaa mguu sawa akajitokeza na kutangaza kuwa anarudi CCM je ni kweli alikuwa na dhamira ya dhati kuwatumikia watanzania au alirudi CCM baada ya lengo lake kushindikana huko alikokuwa anapita?

No comments:

Post a Comment