Wednesday, September 22, 2010

WANACHADEMA MUSOMA WAHOFIA MBUNGE WAO KUHUJUMIWA NA CCM

MUSOMA

VIONGOZI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA mjini hapa wamehofia mgombea ubunge wa chama hicho Vicent Nyerere kuhujumiwa na watu wanaosadikiwa kuwa wametumwa na baadhi za viongozi wa Chama Cha Mapinduzi.




Akiongea katika mkutano wa hadhara ambao ulifanyika jana katika mtaa wa Mukendo mjini hapa ambapo Nyerere pia anagombea nafasi ya udiwani katika kata hiyo,katibu mwenezi wa Chama hicho wilaya ya Musoma mjini Nyamhanga Chacha alisema kuwa  tayari wamepata taarifa za ndani kutoka katika Chama cha Mapinduzi ambapo inasemekana chama hicho kimemtuma mtu ambaye walimtaja kwa jina moja Nyaruba ili amdhuru mgombea huyo.

Katibu huyo alisema kuwa siasa ni maisha ya watu hivyo mtu huyo hasijaribu kufanya hivyo   kwani kwa kufanya hivyo atakuwa anahatarisha maisha yake na si maisha ya mbunge huyo kama wanavyodhani,aliongeza kuwa hali hiyo inatokana na chama hicho kuwa na mwenendo mzuri katika jimbo hilo hivyo kuuwa nguvu hizo CCM wanataka kuleta mchezo mchafu.

  "Ndugu zangu wanachadema kuna kitu ambacho nataka niwaeleze ili nanyi mjue,kuna mtu mmoja anaitwa Nyaruba huyu ni mtu wa chama cha Mapinduzi ambaye jana alikaa na mmoja wa viongozi huko jijini Dar es Salaam wakipanga jinsi ya kuja kumhujumu Nyerere ili CCM ipate unafuu katika jimbo hili na mtu huyo anakuja kesho kutoka Dar sasa nasema mtu huyo ajue siasa ni maisha ya watu hasijaribu kufanya chochote maana atajikuta anakuwa maiti" alisema katibu huyo.

Akihutubia katika mkutano huo mgombea ubunge kupitia chama hicho Vicent Nyerere alisema kuwa nguvu ya umma ya chama hicho ipo kamili kwani kilichopangwa na Mungu kamwe hakibadilishwi na binadamu.

Alisema taarifa hizo ni kweli walizipata hivyo nao wanamsubiria mtu huyo ambaye atarejea mjini kesho yaani leo mjini hapa kutoka Dar es Salaam ili waone kama ataweza kufanya kile walichomtuma na viongozi hao wa CCM.

  "Taarifa tumezipata nasi tunasubiria kuona kama mtu huyo ataweza kupambana na nguvu ya umma,maana sisi tunamtegemea Mungu na si Majini"alisema Nyerere

Aidha katika kuomba ridhaa kwa wananchi mgombea huyo alisema kuwa kama atapata nafasi hiyo kwa miaka mitano ataishauri serikali kuleta wtaalamu wa masuala ya akina mama na watoto katika hospital ya mkoa wa Mara ili kupunguza vifo vya watoto na wakina mama.

Alisema akiwa kama mbunge hawezi kuona watu wanakufa pasipo sababu eti kwa kukosa wataalam ambao serikali ni wajibu wao kuhakikisha wanalinda watu wao katika idara zote ikiwemo na afya.

Kwa upande wa Magereza Nyerere alisema kuwa kwasasa Magereza ya Musoma mjini imekuwa ikiweka watu kitu ambach kinaweza kusababisha magonjwa mbalimbali katika magereza hayo,alisema kuwa magereza yamekuwa na uwezo wa kubeba watu zaidi ya elfu 22 lakini kwa sasa Magereza ya Musoma yamekuwa yakiweka wafungwa zaidi za elfu 45.

  " Jamani Magereza yetu hayaridhishi hivyo tuna kila sababu ya kufanya maboresho kwani kama hatutafanya hivyo basi kila siku kutakuwa na magonjwa ya mlipuko kwa wafungwa na askari lazima tuyarekebishe"alisema mgombea huyo.

Akiongelea suala la Mwenge wa Uhuru mgombea huyo alisema kuwa lengo la mwasisi wa Taifa hili Hayati mwalimu Julius Nyerere ambaye ni baba yake mkubwa ilikuwa ni kuleta matumaini palipopotea na upendo pale penye chuki lakini leo Mwenge huo alisema umekuwa ni kitega uchumi cha watu wachache katika nchi hii,alisema kuwa kuna kila sababu ya serikali kufanya tathimini upya ili mwenge huo utumike kama ilivyokuwa makusudio ya Baba  wa Taifa na si vinginevyo.

Akigusia sekta ya michezo Nyerere alisema kuwa mipango itapangwa ili kufufua micheyo katika jimbo hilo kwani kwasasa michezo imetoweka wakati katika dunia ya leo michezo ni ajira yenye kuleta neema katika familia.

,..........................................................................................................................

No comments:

Post a Comment