Friday, September 17, 2010

TUCHAGUE VIONGOZI MAKINI--DP

MUSOMA

CHAMA cha Democratic Party kimesema kuwa kama watanzania hawatamchagua kiongozi makini ambaye kweli anadhamira ya dhati ya katika kuikomboa Tanzania basi kuna kila sababu ya mzawa katika nchi hii akaishi kama mkimbizi huku wachache wakijinufaisha na maliasili ya Tanzania.

Hayo yalisemwa hivi karibuni na mgombea ubunge jimbo la Musoma mjini kupitia chama cha Demokratic Party Christant Ndege Nyakitita kinachoongozwa na mchungaji Christopher Mtikila wakati akizindua kampeni za chama hicho katika viwanja ya Kamnyonge mjini hapa.

Alisema kuwa kama atapata ridhaa ya wanaMusoma kwa miaka mitano atahakikisha anapambana na masuala ya elimu,afya na miundombinu kwani kukosekana kwa elimu ndio chanzo cha mzawa kukosa haki yake katika jamii ya kitanzania.

 “Kama wanaMusoma watakubali na kunipa ridhaa ya miaka mitano nasema sitawaangusha kwani sera ya chama chetu ni kuangalia kwanza wazawa kwani hakuna sababu ya mzawa kupata tabu wakati nchi yake ni tajiri na hivyo ndivyo nitafanya kwa jimbo la Musoma mjini”     

Nyakitita alisema kuwa jimbo la Musoma mjini limekuwa na kero nyingi ambazo wabunge waliopita wameshindwa kuzitatua hivyo ni vyema wananchi wakafanya mabadiliko ili kulikomboa jimbo hilo n kizazi kijacho.

Alisema suala kama la maji ni aibu kwa mji kama huo kuwa bado kero wakati ziwa Victoria liko mita chache kutoka kwenye makazi ya watu lakini mzawa amekuwa bado katika hali ya sintofahamu kuhusu maisha ya kesho.

Mwenyekiti huyo wa chama cha DP mkoa wa Mara alisema kuwa mbali na maji kuwa kero lakini suala la ujinga,maradhi na umaskini pia ni tatizo katika jamii ambapo alisema tayari yeye na chama chake wamejipanga kupambana nayo.

 ‘Leo suala la maji ni tatizo kwa makazi wa Musoma huku ziwa Victoria liko mita chache kutoka katika makazi ya watu,lakini hii yote inatokana na ujinga ambao watanzania umewazunguka hasa viongozi wasioweza kufikiri,nipeni hiyo nafasi muone nini DP itafanya” alisema Nyakitita 

Aliongeza kuwa anajua watu wengi watakuwa wakiuliza ni wapi atapata fedha ya kufanya hivyo lakini ana imani kuwa fedha ambazo zinatolewa katika mfuko wa jimbo ni msaada tosha kwa mbunge kushirikiana na wananchi huska katika kutafuta maendeleo.

 Mgombea huyo alisema ni kweli leo kijana wa kitanzania anaweza kusoma bure kuanzia ngazi ya chini mpaka chuo kikuu kwani suala hilo ni mipango ya viongozi kama kweli watakuwa na dhamira ya dhati kufanya hivyo,aliuliza mbona wakati wa utawala wa mwl Nyerere watu walisoma bure?

Alisema ili kuinua kiwango cha elimu katika jimbo la Musoma mjini atahakikisha watoto wa jimbo hilo wanasoma bure kwa kuondoa michango yote katika shule za jimbo hilo na kazi itakuwa moja kwa vijana kwenda shule.

Katika suala la Afya mgombea huyo alisema kuwa kama atapata nafasi hiyo hospital ya Kwangwa ambayo ilianza kujengwa miaka ya themanini ujenzi wake utaanza ndani ya siku mia moja na kama haitakuwa hivyo basi wanaMusoma wana kila sababu ya kumtoa katika nafasi hiyo.

Alisema jimbo hilo ni kubwa hivyo ni bora likapata hospital kubwa ambayo itakuwa msaada kwa watu wa jimbo hilo na majimbno jirani,aliongeza kuwa DP ni chama makini ambacho lengo ni kumkoa Mtanzania katika makucha ya mafisadi.

Aidha katika hatua nyingine mgombea huyo wa ubunge katika jimbo la Musoma mjini aliishuku taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa kwabi alisema kuwa taaisis hiyo ni genge la kujipatia fedha kwa watu wenye fedha.

 ‘Jamani hii Takukuru ni genge la kujipatia fedha kwa baadhi ya watu maana wanapigiwa simu kuwa kuna mgombea ametoa rushwa ili mtu ajitoe katika kugombea nafasi Fulani lakini na wao wakifika wanapewa fedha wanakaa kimya sasa kweli ina msaada wowote hii Takukuru katika jamii?” alihoji mgombea huyo

Alisema kuwa kwa leo ni vigumu kwa vya vya upinzani kuungan kwani katika sheria ya nchi hakuna sehemu ambayo inawashinikiza viongozi wa chama hicho kufanya hivyo,Nyakitita aliongeza kuwa pamoja na wananchi kuhoji juu ya hilo lakini pia wana nafasi ya kuchagua chama cha upinzani pasipo kuungana

Katika jimbo la Musoma mjini jumla ya wagomea watano wanagombea nafasi hiyo ya ubunge katika uchaguzi mkuu mwka huu ambao ni Mstapha Wandwi (CUF).Vicent Nyerere (CHADEMA),Vedastus Mathayo (CCM), Tabu Said (NCCR Mageuzi) na Christant Nyakitita(DP)




No comments:

Post a Comment