MUSOMA
MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Musoma Mjini mkoani Mara kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Vincent Nyerere ameendelea kuwa na ushawishi mkubwa kwa wananchi mjini hapa huku akitia kiwewe wagombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na CUF kutoka na kusema yuko tayari kuliokoa jimbo la Musoma kwa kufufua viwanda.
Mbali na ahadi hizo kwa wananchi Nyerere pia ameahidi kutoa msaada katika makundi maalum ndani ya jamii hasa walemavu,watoto wanaishi katika mazingira magumu kwa kupata elimu hadi chuo Kikuu, kuwasaidia Wazee na Wastaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kupata mafao
yao kutoka Serikalini ambayo siku hadi siku yamekuwa ni danadana.
Nyerere alisema kuwa uongozi wake kama mbunge wa jimbo la Musoma mjini atahakikisha kunakuwepo mpango maalum kwa wanafunzi wote wanahitimu elimu ya msingi na kushindwa kupata bahati ya kujiunga na Sekondari kujiunga elimu ya ufundi katika vyuo vya VETA ili kufanya vijana hao wajiendeleze katika maisha yao.
Mgombea huyo amekuwa akitoa ahadi hizo katika mikutano yake ya kampeni ambapo juzi akiwa katika kata wa Kamnyonge maeneo ya marie stopers ambapo umati mkubwa wa wananchi walijitokeza kumsikiliza,mgombea huyo wa ubunge wa Chadema ambaye ni mtoto Kiboko Nyerere mdogo wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere .
Alisema kuwa endapo atachaguliwa kuwa mbunge kazi ya kwanza katika kuhakikisha watoto wanapata elimu bora atapiga marufuku
wanafunzi kutumikishwa shuleni kwa kazi kulima, kutumikishwa katika nyumba za walimu na michango ya shule ya maji,ulinzi na umeme ambayo imekuwa kero kubwa kwa wazazi wa jimbo la Musoma mjini
Nyerere tangu ateuliwe na chama chake kugombea ubunge jimboni Musoma mjini na kuonekana kuwa gumzo kubwa kutokana na kukubalika kwake jimboni
humo katika rika mbalimbali na kupewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi.
Jimbo la Musoma tangu kuanza kwa uchaguzi wa vyama vingi limekuwa likiongozwa na CCM na kuwa na historia mbunge kutoliongoza kwa vipindi viwili na endapo Mathayo atashinda uchaguzi huo atakuwa amejenga historia mpya,katika mkutano wa juzi maeneo ya Kamnyonge Marie stoppers Nyerere alisema kuwa katika uongozi wake atahakikisha viwanda vinafufuliwa ili wananchi wa jimbo hilo waweze kupata ajira
Aidha katika suala la Masoko alisema kuwa ataboresha masoko katika mji huo, na ataruhusu wajasiliamali wadogo wakiwemo mama ntilie kufanya biashara zao bila bughuza za kulipishwa ushuru huku vijana wakipewa mitaji katika vikundi ili kuinua kipato chao
Pamoja na mambo ya masoko lakini pia mgombea huyo alihaidi wananchi wa jimbo hilo kuwa iwapo Chadema kitaingia madarakani,
itarudisha kwa wananchi fedha za DEC zilizozuiliwa na Serikali.
Akimalizia mkutano huo Nyerere alisema kuwa umaskini wa Tanzania unasababishwa na Chama cha Mapinduzi hivyo wananchi lazima wakubali mabadiliko kwani ndio matumaini pekee ya maendeleo katika jamii ya watanzania.
No comments:
Post a Comment