MWENYEKITI wa chama cha wananchi CUF wilaya ya Musoma mjini amenusurika kufa baada ya kujeruhiwa vubaya kwa kipigo kutoka kwa watu aliwataja kuwa ni wafuasi wa Chama cha mapinduzi (CCM) jimbo la Musoma mjini.
Didi Msira Koko
Mwnyekiti huyo wa CUF Didi Msira Koko ambaye pia ni mgombea udiwani wa kata ya Iringo katika Manispaa ya Musoma alipatwa na mkasa huo jan jioni baada ya mkutano wa kampeni wa mgombea urais kupitia chama chama Mapinduzi CCM Jakaya Kikwete katika uwanja wa shule ya msingi Mukendo.
Koko ambaye kwa sasa amelazwa katika katika hospitali ya serikali ya mkoa wa Mara hodi namba mbili,alisema kuwa baada ya kumalizika mkutano huo wa kampeni alianza kuondoka kwenda kwake maeneo ya Iringo lakini ghafla aliitwa na kundi la vijana ambao ni ndugu na wafuasi wa mgombea ubunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo na kuanza kumuuliza juu ya sera za CCM.
Didi Msira Koko
Alisema kuwa baada ya kuwajibu kuwa sera kila chama kinazo hivyo ni wakati wa kusikiliza kwanza kisha mwananchi mwenyewe ndiyo ataamua na hapo ndipo kipigo kilipoanza.
‘Waliniita wakati natoka kwenye mkutano wa Jakaya wakaanza kuniuliza sera za CCM mimi niliwaeleza kila chama kina sera na mwananchi atasikia ni sera ya chama gani nzuri na kuamua kuipa kura ,sasa wakati nasema hivyo ndipo kijana mmoja anaitwa Mapinduzi aliponivamia na kuanza kunipiga eti kisa nampinga Mathayo”alisema mwenyekiti huyo
Kamanda wa polisi mkoani Mara kamishina msaidizi Robert Boaz kizungumza na Jambo Leo kwa njia ya simu alisema kuwa leo walikuwa na pilika za kumsindikiza mgombea urais wa CCM Jakaya Kikwete ingawa bado jeshi hilo linafanya uchunguzi kujua chanzo cha mwenyekiti huyo wa CUF kuvamiwa na kupigwa.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa vijana waliompiga waliokuwa wamevalia sare za CCM ambapo aliongeza kuwa baada ya kuokolewa na wananchi punde gari la polisi lilitokea ambalo lilimbeba na kumfikisha kituoni kwa kupewa fomu namba tatu ya matibabu (PF 3) na kupata msaada wa kufikishwa hospitalini hapo kutokana na kushindwa kutembea baada ya mguu huo wa kulia kuumizwa vibaya ingawa baada ya kupiga X-ray ulionekana kuna mfupa umehama lakini haukuvunjika.
Naye mgombea ubunge wa chama cha Demkrasia na maendeleo (CHADEMA) Vicent Nyerere akiongelea tukio
Mgombea huyo alisema kuwa vitendo vingi vya fujo mjini hapa vinasababishwa na genge la watu wa Chama cha Mapinduzi hivyo
Aidha majira ya saa saba mchana mwandishi wa gazeti hili alifika katika hospital ya mkoa wa Mara ili kumjulia hali kiongozi huyo wa CUF ambapo alisema hali yake si mbaya
‘Nashukuru
Mwenyekiti huyo ambaye leo alikuwa na mkutano wa hadahara katika kata yake alisema kuwa kuvamiwa na vijana hao kunaweza kuathiri mikutano yake ya kampeni.
No comments:
Post a Comment