Salaam kwako, Wahandishi wote. Mimi na familia yangu hapa Seoul- Korea tunaendelea vizuri sana na maisha, kazi, na masomo. Kwanza napenda nikushukuru kwa kuniandiakia message hii. Pili, nashukuru kunijulisha mambo yalivyo Musoma na hali ya kisiasa kwa ujumla kama blog yako inavyo onyesha.
Challenge Musoma Change
Eliud Esseko Tongola (Mkorea
Tangu nirudi Korea mambo mengi mazuri yametokea. Kuna uwezekano mkubwa wa mimi kuendelea na masomo ya Post Doctoral Studies baada ya Ph.D. Graduation hapo February 2011. Hii Program ni ya miaka miwili na haipo katika vyuo vya Tanzania. Pia nimepata nafasi ya kusoma Ph.D Nyingine kwenye fani ya World View (Hapa Seoul au Denmark). Mbali na hayo, Nakamilisha ujenzi wa shule yangu ya Bweni hale Kibaha; itachukua wanafunzi 1200 na itafunguliwa January 2011.
Kabla ya 2015, nitakuwa nimeisha jenga shule ya kisasa ya bweni hapo Musoma, nitakuwa na nyumba yangu ya kisasa hapo Musoma na nitashughulikia baadhi ya miradi kama nilivyo hainisha kwenye vipeperushi vyangu. Kwa ujumla, Wakorea wananihitaji sana sana niendelee kufundisha katika vyuo vikuu hapa, lakini moyo wangu na upendo wangu upo Musoma (Musoma Refomata Videre; the Vision to transform Musoma). Siwezi kusahau Challenge Musoma Change, it's real and it will be in God's appointed time.
Mwisho nawatakia uchaguzi mwema na wa amani. Ni maombi na dua zangu kwamba uchaguzi ufanyike salama. Nisalimie mgombea udiwani wa CUF ambaye amelazwa hospitalini. Namtakia kupona haraka na awe na afya njema. Waambie wanamusoma tuombee amani na usalama na tudumishe amani na usalama.
Wadadisi wa mambo ya siasa mkoani hapa wanadai kuwa kama huyu angesimama katika nafasi hiyo CCM wasingekuwa na hali ngumu kama ilivyo sasa.
Wadadisi wa mambo ya siasa mkoani hapa wanadai kuwa kama huyu angesimama katika nafasi hiyo CCM wasingekuwa na hali ngumu kama ilivyo sasa.
Mungu ibariki Musoma, Mungu ibariki Tanzania.
Mwana Musoma,
Eliud Esseko Tongola ( Mkorea)
No comments:
Post a Comment