MGOMBEA mmoja wa ubunge wa jimbo la Bunda mkoani Mara,amesema wananchi wanapaswa kuwapuuza wapinzani wanaotumia suala la ufisadi kama mtaji wa kutafutia kura kwa vile jambo hilo ni sawa na kufunga kanisa kwa kosa la kiongozi mmoja dini kukutwa akizini.
Mgombe huo ambaye pia ni mjumbe wa halmashauri kuu NEC ya chama cha mapinduzi CCM,alisema haya juzi wakati wa kuzindua kampeni za chama hicho kwa majimbo ya Bunda na Mwibara.
Alisema kuwa serikali ya awamu ya nne chini ya rais Jakaya Kikwete, ameweza kuchukua hatua kali za kupambana na vitendo vya rushwa na ufisadi na kiliweka taifa katika mstahili hivyo hakuna sababu ya wapinzani kutumia hoja hiyo kama mtaji badala ya kueleza sera za vyama vyao.
"Kila leo mtu mzima akilala na kuamka anaimba ufisadi hivi kama Padri mmoja amekutw akizini tunafulinga kanisa? kinachofanyika ni kumshughulikia kwa kulingana na taratibu huku wauumini wakiendelea na ibada na hivyo ndivyo rais wetu anavyofanya kwa yoyote anatuhumiwa na vitendo hivyo anafikishwa katika vyombo vya sheria bila ya kumuonea mtu aibu je hawa wenzetu wanataka rais akiambiwa huyu ni fisadi atoe amri ya kunyongwa bila ya kumfikisha mahaksama"alihoji Wassira na kushangiliwa.
Wassira ambaye ni waziri wa kilimo,chakula na ushirika,alisema mafanikio makubwa ya serikali ya awamu ya nne yametokana na rais Kikwete kulelewa vema na Baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere hatua ambayo imemuwezesha kuliongoza taifa kwa misingi mizuri kwa kujali maslahi ya taifa.
Alisema inasikitisha kuona baadhi ya vyama vya upinzani kuchukizwa na sera ya serikali ya awamu ya nne kwa kutoa ruzuku katika pembejeo za kilimo huku wakiishiniza serikali kuwauzia wakulima pembejeo hizo kwa bei ya juu na hivi sasa wamejitokeza sasa kuomba kura za wakulima hao.
"Serikali ya CCM imekuwa ikichukizwa baadhi ya wapinzani kulaani vikali mpango wa kuwapa wakulima ruzuku katika pembejeo za kilimo na watu hao hao leo wamejitokeza kuomba kura za wakulima..sisi tumesema tutazidi kuwasaidia wakulima kuliko ilivyo hivi sasa hadi kufikia hatua ya kuachana na matumizi ya jembe la mkono"alisema.
Alisema kutoka na sera hiyo nzuri ya akiwa kiongozi wa wizara ya kilimo,katika msimu huu wa zao la pamba wizara yake imetangaza kila mnunuzi wa zao la hilo atapaswa kununua kilo moja kuanzia shilingi mia sita na endapo itabainika kukiuka agizo hilo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
Alisema kuwa hivi sasa serikali ya CCM imejipanga kikamilifu kubadili hali ya kilimo ili sekta hiyo iweze kubadili hali ya uchumi kwa kuanzisha benki ya wakulima ambayo pia itawawezesha wakuluma kupata mikopo ya kuendeshea kilimo hicho cha kisasa.
"Hatuwezi kujenga uchumi wa kisasa bila kufanya mabadili makubwa katika sekta ya kilimo na hivi ndivyo tuvyosema sisi CCM..tumejipanga kufanikisha yote haya"alisema.
Wassira alisema kuwa wananchi wana kila sababu ya kukipa chama hicho kura za kishindo katika uchaguzi wa oktoba 31 ili kuweza kukamilisha kazi nzuri zilizoanza kutekelezwa na serikali ya awamu ya nne hasa ujenzi wa nyumba za walimu,maabara,zahanati kila kijiji na vituo vya afya kila kata.
Aliwaomba wananchi hao wa jimbo la Bunda kumchagua kuwa mbunge ili aweze kutekeleza miradi mikubwa ya maji ambayo ameanza kuitekeleza ikiwa ni pamoja na kuchagua madiwani wa CCM pamoja na kumpigia kura nyingi mgombea wa urais wa chama hicho.
"Kwa muda mfupi tu ujao endapo mtatupa ridhaa kwa mara nyingine suala la maji katika wilaya ya Bunda litakuwa ni historia kwani kwa miaka mitano tu tumechimba zaidi ya visima 30 mabwawa makumbwa ya maji kwaajili ya binadamu na mifugo na sasa mradi mkubwa wa zaidi ya bilioni kumi unatekelezwa katika mji wa Bunda haya yote yatawezekana kutokana na sera nzuri ya ccm"alisema.
Mjumbe huyo wa NEC ambaye ni mgombea mbunge wa jimbo la Bunda alitumia nafasi hiyo kusema kuwa atalazimika kuongeza nguvu ya kampeni katika jimbo la Mwibara na baadae kuelekea jimbo la Tarime ili kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi wa kishindo katika majimbo hayo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment