Mwezeshaji wa Mafunzo ya uboreshaji wa uandishi wa habari katika Mitandao (Blog) kutoka Mfuko wa vyombo vya habari Tanzania (TMF) Beda Msimbe Kulia akitoa ufafanuzi huku akisikilizwa na Mwezeshaji mwenzake Bw Saimon Mkina katikati
Waandishi wa habari nchini wametakuwa kuwa wakweli katika
kuandika habari mbalimbali wanazoziandika zikiwemo za Uchunguzi katika kusaidia
Jamii inayowazunguka.
Hayo
yameelezwa na Mwezeshaji wa Warsha ya siku tano ya Uboreshaji wa Uandishi wa
habari katika Mitandao ya Kijamii Bw
Simon Mkina Mkoani Dodoma.
Alisema mafunzo
hayo ambayo yameandaliwa na Mfuko wa vyombo vya habari
Tanzania (TMF) yameelezwa yatakuwa Msaada Mkubwa kwa Wanahabari wanaoandika
katika Mitandao ya kijamii kwani asilimia kubwa ya wanahabri kwasasa wamekuwa
wakitoa taarifa za Matukio badala ya kufanya uchunguzi.
Bw Mkina
alisema kuwa uandishi wa habari za Uchunguzi utakuwa na Msaada Mkubwa katika Jamii kwani
kinachotakiwa na mhusika kuandika vitu vya kweli na kufuata maadili ya uandishi
wa habari.
Katika
hatua nyingi Mkina alitaka wanahabari hao na
wengine ambao hawajapatiwa mafunzo ya uboreshaji wa habari za
mkitandaoni ni vema sasa kurejea katika maadili .
Kwa
upande wale mkufunzi wa mafunzo
hayo Bw Beda Msimbe alisema kuwa lengo la kuanzisha mafunzo
hayo ambayo ni ya kwanza kufanyika ni kutoka kuongeza ubora
wa uandishi unaozingatia maadili katika mitandao hiyo .
Msimbe
alisema kuwa usalama wa wanahabari utaendelea kuwa
hatarini iwapo wanahabari hawataheshimu maadili na kuendelea
kutumika kwa kuchafua ama kufanya uandishi usio
zingatia maadili.
Kwa
upande wake afisa miradi wa TMF Japheth Sanga aliwataka
wanahabari hao mbali ya kuandika habari za uchunguzi kuhakikisha
wanaheshimu sheria za nchi .
No comments:
Post a Comment