VIONGOZI WA VYAMA VYA WAANDISHI WA HABARI KUTOA
TAMKO JUU YA KIFO CHA DAUDI MWANGOSI
Mwenyeviti
na Makatibu wa vyama vya
waandishi wa Habari Mikoa Mbalimbali Tanzania
Wanaanda Utaratibu wa Kutoa tamko juu ya Waandishi waliopo katika Vyama
hivyo kutoa tamko kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi
wa habari mkoa wa Iringa Daudi Mwangosi.
Mwenyekiti wa MRPC (MARA) Bw Emmanuel Bwimbo
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka jijini Dar es
Salaam,Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Mara (MRPC)
Emmanuel Bwimbo amesema kuwa katika
mkutano utakaofanyika kesho katika hotel ya Lion viongozi hao wamekusudia kutoa tamko juu ya
kifo cha Daudi Mwangosi mikononi mwa Polisi.
Bwimbo amesema kuwa kusudio lao kubwa ni kutoa tamko
la wanachama wa Vyama hivyo ambao waandishi wa habari kutofanya kazi pamoja na
Jeshi la Polisi hapa nchini kama wahuska katika tukio hilo hawatachukuliwa
hatua
Amesema ni unyama mkubwa ambao Jeshi la Polisi
wamefanya kwa Mwenyekiti huyo wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Iringa
hivyo ni bora nao wakachukua hatua.
“Hapa mimi
nadhani kesho lazima tutoe tamko juu ya hawa waliohusika katika Unyama
huu,haiwezekani Mwandishi Daudi akafa
mbele ya Polisi na hao Polisi wakashindwa kuchukuliwa hatua haiwezekani”?
No comments:
Post a Comment