Moja Wa Vilabu Vya Waandishi Wa Habari Tanzania Yatoa Tamko Kuhusiana Na Mauaji Ya Mwandishi Daudi Mwangosi Mkoani Iringa

UMOJA
wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC)umesema kuwakufuatia
mauaji ya mwandishi wa habari wa Wa kituo cha Channel Ten Mkoani Iringa
Bw. Daudi Mwangosi kimeitaka serikali kuwasimamisha kazi askari
waliohusika katika tukio la mauaji ya kinyama ya mwandishi huyo. Umoja
huo umesema kuwa askari walioshiriki katika oparesheni hiyo ambayo ni
haramu kusimamishwa mara moja ili kupisha uchunguzi kufanyika.
Hayo
yalisemwa jana Jijini Dar Es Salaam na Rais wa UTPC Bw.Keneth Simbaya
wakati alipokuwa akitoa tamko Kwa Viongozi wa Vilabu Mikoani kuhusiana
na mauaji dhidi ya mwandishi wa habari Huyo aliyeuwawa akiwa mikononi
mwa polisi katika kijiji cha Nyololo Wilayani Mufindi. “Hapa tunataka
uchunguzi huu ukikamilika tunaitaka serikali kuutangazia umma na kupisha
sheria kwa wale watakaobainika kuhusikakwa uzembe huo kwa namna moja au
nyingine wachukuliwe hatua dhidi ya mauaji hayo ya mwandishi wa habari
Bw. Daudi Mwangosi”alisema.
Hata
hivyo Bw. Simbaya alisema wakati uchunguzi ukiwa unaendelea serikali
iridhie na kurasimisha malipo kwa ajili ya Mjane wa mwandishi huyo na
watoto walioachwa na marehemu ili waweze kujikimu.
Aidha
alisema licha ya kutoa tamko hilo wanaendelea kulitazamia jeshi la
polisi kama mdau mwenye shaka kwa namna wanavyotenda kazi zao na
waandishi wa habari mikoani na kwamba watataarifu umma kuhusu
mwenendo
wao hapo baadae. “Lakini pia katika mkutano huu tumeridhia kushirikiana
na taasisi zingine za haki za binadamu ,uwakili na Utetezi ili kubaini
namna bora ya kuishitaki serikali kama mwenendo wa suala hili hautakuwa
unaleta tija Kutokana na vithibitisho hivyo tunakaribisha mashirika ya haki za binadamu ,asasi zisizokuwa za kiserikali ili kuweza kufanikisha azma hii”alisema Bw. Simbaya.
Akizungumzia
kuhusu usalama kwa waandishi wa habari Bw. Simbaya alisema katika
kuhakikisha kuwa waandishi wa habari wanafanya kazi yao kwa usalama
amelitaka jeshi la polisi kutoa utaratibu ambao utawezesha
wanahabari nchini kufanya kazi kwa usalama bila hofu wala dharau,kutoa
elimu kwa jeshi la polisi kuhusu umuhimu wa wanahabari na jukumu lao
katika Taifa.
Hata
hivyo baadhi ya viongozi wa Vyama vya waandishi wa habari Tanzania
ambao wanahudhulio mkutano mkuu wa UTPC walisema tamko hilo halijapewa
uzito kutokana na tukio la mauaji lenyewe na jinsi lilivyo huku wakitaka
Tamko hilo kupewa uzito wa kina. “Hili Tamko lilitakiwa kupewa uzito
sana kwani sisi tuliokuwepo katika msiba huo kwa ujumla inasikitisha
sana hivyo tamko ni muhimu lipewe uzito zaidi kulingana na mauaji
yenyewe yanavyotisha hivyo tufuate maamuzi ya viongozi wa clabu waliotoa
matamko ya kususia habari za polisi mpaka pale watakapokuwa wameridhia
kukaa meza moja na wanahabari juu ya mauaji hayo”alisema mmoja wa
viongozi wa clabu za waandishi wa habari Tanzania Bw. Christopher
Nyenyembe.
Habari na Esther Macha Na Mwajabu Kigaza
No comments:
Post a Comment