WANANCHI TARIME WATAKIWA KUJIKITA KATIKA KILIMO
Dinna
Maningo,Tarime
WANANCHI
Wilayani Tarime wametakiwa kujikita katika kilimo cha mazao mbalimbali kutokana na Wilaya hiyo kuwa na misimu miwili
ya kilimo na kuwa endapo watawekeza kwenye kilimo itawasaidia kujiendesha kimaisha wao na familia zao.
Akiongea na ofisini kwake Ofisa kilimo wa Wilaya ya Tarime Selvanus Gwiboha
alisema kuwa Wilaya ya Tarime ina uhakika wa chakula kwa mwaka na ardhi yenye rutuba ya kutosha ambapo
alisema kuwa katika msimu huu wa masika Wilaya inatarajia kuvuna tani 180,106 nakuwa msimu wa vuli utaanza
Septemba 2012 hadi Januari 2013.
“wananchi
wawekeze kwenye kilimo wasibweteke,kilimo ni uti wa mgongo watu wasiache kulima
mazao yanafaida kubwa unauza na unayatumia
kwa chakula na mahitaji mengine,mazao yanayolimwa Tarime ni
mihogo,mahindi,mtama,ulezi,mpunga,viazi vitamu,viazi mviringo na maharage na kwa
upande wa mazao ya biashara ni kahawa na ndizi na mikakati inawekwa kulima
alizeti na ufuta”alisema
Gwiboha.
Gwiboha alisema
kuwa kwa Wilayani hapa eneo linalofaa kwa kilimo ni Hekta 790,630 ambapo eneo
linalolimwa ni Hekta 69,155 sawa na asilimia 76.30 eneo linalofaa kwa kilimo.
Alisema kuwa
eneo linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji ni Hekta 8,643 na linalolimwa ni
Hekta 6 sawa na asilimia 0.07 nakwamba zana zilizopo ni matrecta 12 ndiyo pekee
hutumika kwa shughuli za kilimo huku plau zilizopo ni 9,495.
Gwiiboha
aliongeza kuwa kwa upande wa upokeaji na usambazaji wa vocha za pembe jeo
Wilayani Tarime ilipokea jumla ya Vocha 18,000 za kutosheleza wakulima 18,000
sawa na ekari 18,000,mbolea tani 18,000,Urea tani 18,000 na mahindi chotara
tani 18,000 nakwamba thamani ya vocha zote ni 1,296,000,000, pia jumla ya
vijiji 89 vimenufaika na ruzuku za pembe jeo.
No comments:
Post a Comment