SERIKALI
YATAKIWA KUTUMIA MIKUTANO KUHAMASISHA WANANCHI KUHESABIWA.
Dinna
Maningo,Tarime
BAADHI ya
wananchi Wilayani Tarime wameitaka Serikali kuwatumia viongozi wa serikali za
vijiji na kata kupitia mikutano ya hadhara ili kutoa elimu ya uhamasishaji wa
wananchi kuhesabiwa katika sensa na makazi.
Hayo
yameelezwa kwenye kongamano lililoandaliwa
na Chama cha Democrasia na Maendeleo Chadema (CHADEMA )Kata ya Sabasaba
lililofanyika ukumbi wa J.J CLUB leo lililowakutanisha wananchi mbalimbali
mjini Tarime lililokuwa linahusu
kuhamasishaji wa wananchi kujitokeza katika zoezi la sensa na makazi.
Wananchi wamesema
kuwa licha ya Serikali kutoa matangazo,vipeperushi na kutangaza kupitia vyombo
vya habari juu ya umuhimu wa sensa bado haitoshi kutokana na kuwa wakazi wengi waishio
vijijini hawafikiwi na matangazo hayo na wengine wakiwa hawana redio jambo
ambalo linaweza kusababisha watu wasijitokeze kwenye sensa kutokana na kutojua
umuhimu wake.
Hivyo wamewataka
viongozi wa vijiji na kata kutoa elimu kupitia mikutano ya wananchi juu ya
umuhimu wa mtu kuhesabiwa na kuwa kufanya hivyo itasaidia Serikali kupata idadi
kubwa ya watu waliojitokeza kuhesabiwa.
Zacharia
Ghati mkazi wa Ronsoti Mjini Tarime amesema kuwa uhamasishaji ni muhimu
kwani unasaidia wananchi wote kuelewa umuhimu wa sensa
ili waweze kutoa ushirikiano na kushiriki katika zoezi zima la sensa
Hata hivyo
wananchi wameiomba serikali wakati zoezi
la nsensa litakapokamilika takwimu za
idadi ya watu zitumike ipasavyo na sio kutunzwa bila kufanyiwa kazi kwa madai
kuwa katika sensa iliyopita haijasaidia kutokana na kuwa baadhi ya huduma za
jamii zimeshindwa kuboreshwa hususani katika swala la kuhakikisha wanafunzi
wanapata elimu bora kama vile vitabu vya kutosha mashuleni jambo ambalo
limeshusha taaluma kwa wanafunzi.
No comments:
Post a Comment