VIONGOZI MBALIMBALI WAJITOKEZA KUMUAGA ALIYEKUWA MWENYEKITI WA CHAMA CHA SOKA MKOANI MARA
Michael Wambura mdau wa soka.
Mh Mkono akiaga Mwili wa marehemu
Mkuu wa Mkoa wa Mara Bw John Tuppa akiaga mwili wa Marehemu
Makongoro Nyerere ambaye ni mtoto wa Hayati Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere.
Waziri wa kazi na ajira Gaudencia Kabaka akiwa pamoja na Rais wa TFF leodger Tenga katika mazishi hayo
Wajukuu wa Marehemu
Rais wa shirikisho la soka hapa Nchini (TFF) Leodiger Tenga
ameongoza maelfu ya waombolezaji katika mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti
wa chama cha soka Mkoani Mara (FAM) na mjumbe wa kamati ndogo ya
mahesabu ya (TFF) Fabian Samo yaliyofanyika nyumbani kwake maeneo ya
Nyakato katika Manispaa ya Musoma.
Mkuu wa wilaya ya Bunda Joshua Mirumbe
Katibu mkuu wa chama cha soka mkoani Mara Galibona Kamgisha
Na Shomari Binda
Musoma
Rais wa shirikisho la soka hapa Nchini (TFF) Leodiger Tenga ameongoza
maelfu ya waombolezaji katika mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa chama
cha soka Mkoani Mara (FAM) na mjumbe wa kamati ndogo ya mahesabu ya
(TFF) Fabian Samo yaliyofanyika nyumbani kwake maeneo ya Nyakato katika
Manispaa ya Musoma.
Akisoma salamu za rambirambi kutoka
Shirikisho la soka hapa Nchini,Tenga alisema wamepata pengo kubwa kwa
kuondokewea na kiongozi huyo kwa kile alichokieleza bado mchango na
mawazo ya kiongozi huyo yalikuwa yakihitajika kutokana na uwezo wake
mkubwa aliokuwa nao katika masuala ya mahesabu.
Alisema Samo
alikuwa mwepesi wa kuhudhulia vikao pale alipokuwa akihitajika na
alichangia kwa kiasi kikubwa kuhakikisha uwezo wake aliokuwa nao katika
masuala ya mahesabu anayatoa katika shirikisho hilo na imepelekea kuwa
na uangalizi mzuri katika kusimamia masuala ya fedha.
Tenga
ameeleza kuwa uwezo mkubwa aliokuwa nao Fabian Samo ndio uliopelekea
wadau wa soka katika Mkoa wa Mara kumchagua kwa vipindi viwili
kukiongoza chama cha mpira wa miguu (FAM) na katika kipindi hicho
kumekuwa na mabadiliko makubwa katika soka la Mkoa wa Mara.
Rais huyo wa TFF amewaomba wadau wa soka Mkoani Mara kufata yale yote
mazuri aliyoyafanya marehemu Fabian Samo ili kupitia hayo soka la Mkoa
wa Mara na Tanzania kwa ujumla liweze kundelea na kupanda na kuwaomba
viongozi wengine katika Soka la Mkoa wa Mara kuwa wavumilivu katika
kipindi hiki kigumu cha msiba na kudai kuwa TFF ipo pamoja katika
kipindi hiki cha msiba.
Akitoa salamu kwa upande wa Serikali
kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara John Tuppa ambaye pia alikuwepo
msibani hapo Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Chama
cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara Makongoro Nyerere alisema licha ya
kujishughulisha na kupenda masuala ya michezo marehemu Fabian Samo
alikuwa ni kiongozi mzuri katika masuala ya siasa na kiongozi mvumilivu
tangu alipokuwa Diwani na makamo Mwenyekiti wa Halimashauri ya Wilaya ya
Musoma kwa kipindi cha miaka 10.
Makongoro alisema ili
kumuenzi kiukweli marehemu Fabian Samo ni kufuata yale yote mazuri
aliyoyaacha kwa dhati na kuwa wawazi katika masuala ya uongozi kama
ambavyo alikuwa akifanya kiongozi huyo.
Akizungumza kwa niaba
ya wadau wa soka katika kutoa saramu za rambirambi,aliyekuwa Katibu Mkuu
wa Chama cha soka zamani (FAT) Michael Wambura alisema pengo walilopata
wadau wa soka kufuatia kifo cha Fabian Samo halitazibika kutokana na
moyo aliokuwa nao katika kusimamia masuala ya mpira.
Wambura
alisema ni wajibu wa kila mdau kuiga mazuri yote yaliyofanywa na Fabian
Samo katika kusimamia haki na kuwa wawazi katika kusimamia ukweli ili
kuweza kuendeleza soka la Mkoa wa Mara na Tanzania kwa ujumla.
Viongozi wengine waliohudhulia mazishi hayo ni Waziri wa kazi na na
ajira Gaudensia Kabaka,Mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini Nimrod Mkono,M
kuu wa wilaya ya Bunda Joshua Mirumbe na mstahiki Meya wa Manispaa ya
Musoma Alex Kisulula.
marehemu Fabian Samo alizaliwa mwaka 1944
katika kijiji cha Wegero Wilaya ya Musoma vijijini ameacha mjane,watoto
12 na wajukuu 17.
Mungu ailaze roho ya Marehemu Fabian Samo mahali pema peponi
No comments:
Post a Comment