CHAMA KIPYA CHA SIASA CHA ADC CHAPATA WANACHAMA WA KUTOSHA MARA
Na Shomari Binda Musoma
Wanachama wa vyama vya siasa hapa nchini wametakiwa kuwa wavumilivu
katika hoja za kisiasa ili kuweza kufanikisha dhana ya kuanzishwa kwa
mfumo wa vyama vingi na demokarasia ya kweli katika kufanikisha mfumo
ho.
Kauli hiyo imetolewa na afisa mfawidhi wa katoka ofisi ya
msajili wa vyama vya siasa hapa chini kutoka kanda ya ziwa lodovick
Joseph wakati akisoma idadi ya watu walijitokeza kukidhamini chama kipya
cha siasa hapa Nchini cha allance Democratic Change (ADC) katika ukumbi
wa mikutano wa Musoma club.
Alisema wanachama wa vyama vya
siasa wanapaswa kuwa wavumiliovu katika siasa ili kuendana na malengo ya
kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi na uhuru wa mtu kwenda chama
chochote cha siasa anachoona kinamfaa kujiunga nacho kutokana na sera
zake na mfumo wake.
Lodovick alisema wapo baadhi ya wanachama
wa vyama vyama vya siasa wasio wavumilivu katika siasa za kistaarabu na
kupelekea kuanzishwa kwa vurugu zisizo za msingi na kusababisha madhara
kwa jamii ikiwemo kusababisha usunbufu kwa wanachi wengine katika
shughuli zao.
Alisema Mkoa wa Mara umevuka lengo la wanachama
waliojitokeza kukidhamini chama cha (ADC) ambapo jumala ya wanachama
waanzilishi 250 kutoka wilaya za Mkoa wa Mara walijitokeza kukidhamini
na kuizidi mikoa ya Mwanza,Tanga na Pemba ambapo tayari chama hicho
kimeshakwenda kutafuta wadhamini.
Akizungumza na wanachama wa
chama hicho mara baada ya kutangazwa kuvuka lengo la wanachama
waliojitokeza kukidhamini chama hicho,Kaimu Katibu mkuu wa chama cha ADC
Kadawi Lucas Limbu aliwashukuru wanachama hao kwa kujitokeza kwa wingi
na kuonyesha ni namna gani walivyo tayari kwa ajili kutaka mabadiliko.
Alisema lengo la kuanzishwa kwa chama hicho ni baada ya kuonekana vyama
vingi vya kisiasa vilivyoanzishwa hapa nchini kushindwa kufikia malengo
ya kuanzishwa kwake na kutokukidhi yale ambayo wananchi wanayatarajia
kutoka katika vyama hivyo.
Limbu alidai viongozi wa vyama hivyo
vya siasa katika ngazi ya Kitaifa wamekuwa wabinafsi na kushindwa
kuwashirikisha viongozi wengine katika ngazi za chini katika wilaya hasa
pale chama kinapopata mafanikio na kueleza kuwa chama Cha ADC kitakuwa
mfano wa kuigwa katika kuwashirikisha wananchama wake na viongozi katika
kada zote.
Iwapo chama cha ADC kitakamilisha masharti ya
kuanzishwa kwa chama cha siasa hapa nchini waliyopewa na ofisi ya
msajili wa vyama vya siasa hapa nchini kitakuwa chama cha siasa cha 20
tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.
No comments:
Post a Comment